La nne: Ni wajibu kuheshimu dini ya Uislamu, kuiadhimisha, kutoipunguza au kuikosoa. Ni dini ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) na ni Shari´ah ya Allaah. Haijuzu kwa yeyote kuikosoa dini hii, kuipunguza au kuiongelea kwa maneno ambayo ndani yake kuna kuipunguza au kuichezea shere. Huu ndio wajibu inapokuja kwa Allaah, Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Uislamu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 131
  • Imechapishwa: 17/12/2018