Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
80 – Amesema (Ta´ala):
لَا يُسْأَلُ عَمَّا يَفْعَلُ وَهُمْ يُسْأَلُونَ
“Haulizwi kwa yale Anayoyafanya, lakini wao wataulizwa.”[1]
MAELEZO
Hutakiwi kumuhoji Allaah, kubishana Naye juu ya matendo Yake, mipango na makadirio Yake. Kuwa na adabu na Allaah. Wewe ni mja. Hivyo usijiingize katika kazi Zake (Jalla wa ´Alaa). Allaah haulizwi juu ya yale anayoyafanya, kwa sababu Allaah hafanyi chochote isipokuwa ni kwa hekima. Wakati fulani hekima hiyo inaweza kutudhihirikia, wakati mwingine tunaweza kufichwa nayo. Tunaamini kuwa Allaah hafanyi kitu bure. Anafanya kila kitu kwa hekima, ni mamoja hekima hiyo imetudhihirikia au haikutudhihirikia. Mtu ataulizwa juu ya matendo yake mwenyewe, hatoulizwa juu ya matendo ya Allaah (´Azza wa Jall). Kwa hivyo jishughulishe na yale ambayo utaulizwa kwayo siku ya Qiyaamah, nayo ni matendo yako. Kwa hivyo ni lazima kwa mja kujisalimisha kwa Allaah.
[1]21:23
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 113
- Imechapishwa: 04/11/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)