99. Roho zimeumbwa kabla ya viwiliwili au kinyume chake?

Je, roho ziliumbwa kabla ya viwiliwili au kinyume chake? Kuna maoni mawili juu ya masuala haya yaliyotajwa na Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah na wengineo.

1- Roho ziliumbwa kabla ya viwiliwili. Maoni haya yamechaguliwa na Ibn Hazm na Muhammad Naswr al-Marwaziy.

2- Roho ziliumbwa baada ya viwiliwili. Haya ndio maoni ya Salaf na waliokuja nyuma. Dalili ziko wazi kwa mitazamo mingi. Pindi Allaah alipotaka kumuumba baba wa wanaadamu alimwamrisha Jibriyl kuchukue udongo kwa mkono kisha akaufinya mpaka ukawa mchujo safi wa udongo. Kisha Akamuunda. Halafu akampulizia roho. Kisa hiki kinajulikana na kimepokelewa kwa njia nyingi. Kinathibitisha kuwa Alalah alimpulizia roho kutoka Kwake baada ya kuumba kiwiliwili chake. Imesihi ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika kila mmoja wenu linakusanywa umbile lake tumboni mwa mama yake kwa masiku arubaini. Kisha inakuwa kipande cha damu kwa muda kama huo. Halafu inakuwa kinofu cha nyama kwa muda kama huo. Halafu anatumiwa Malaika kumpulizia roho.”

Hadiyth ni yenye kujulikana. Malaika kumpulizia roho kiwiliwilini ndio sababu ya yeye kupata roho.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 214-215
  • Imechapishwa: 10/12/2016