Miongoni mwa mambo yasiyokuwa na mashaka yoyote ndani yake ni kwamba kushikamana barabara na Sunnah kunamuokoa mtu kutotumbukia ndani ya Bid´ah na upotevu. Amesema (Ta´ala):

وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ

“Na kwamba hii njia Yangu iliyonyooka, hivyo basi ifuateni na wala msifuate njia nyenginezo zitakufarikisheni na njia Yake!”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameyaweka hayo wazi katika yale yaliyopokelewa na Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) pale alipoeleza:

“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipiga msitari na akasema: “Hii ni njia ya Allaah” kisha akapiga misitari kuliani na kushotoni na akasema: “Hivi ni vijia; katika kila njia kuna shaytwaan anayelingania kwayo” halafu akasoma:

وَأَنَّ هَـٰذَا صِرَاطِي مُسْتَقِيمًا فَاتَّبِعُوهُ ۖ وَلَا تَتَّبِعُوا السُّبُلَ فَتَفَرَّقَ بِكُمْ عَن سَبِيلِهِ ۚ ذَٰلِكُمْ وَصَّاكُم بِهِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ

Yule anayeipa mgongo Qur-aan na Sunnah atashika vijia vya Bid´ah zilizozuliwa.“Na kwamba hii njia Yangu iliyonyooka, hivyo basi ifuateni na wala msifuate njia nyenginezo zitakufarikisheni na njia Yake! Hivyo ndivyo Alivyokuusieni kwayo mpate kumcha Allaah.”[2]

Sababu zilizopelekea kudhihiri kwa Bid´ah zinafupika katika mambo yafuatayo:

1- Kuwa na ujinga juu ya hukumu za dini.

2- Kufuata matamanio.

3- Kufanya ushabiki juu ya maoni na watu.

4- Kujifananisha na kuwafuata kichwa mchunga makafiri.

Tutatoa maelezo kiasi juu ya mambo haya:

[1] 06:153

[2] Ahmad (4225).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 186
  • Imechapishwa: 02/07/2020