94- Inafaa katika kaburi kufanya mwanandani ulio karibu na ukuta upande wa Qiblah[1] na mwanandani katikati ya kaburi[2] kwa vile matendo mawili yote yamefanywa katika zama za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini la mwanzo ndio bora zaidi. Kumepokelewa Hadiyth kadhaa juu ya hilo:

Ya kwanza: Anas bin Maalik amesema:

“Wakati alipofishwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) al-Madiynah kulikuweko na mtu mmoja anayefanya Lahd na mwengine anafanya Shaqq. Wakasema: “Tumtake shauri Mola wetu na tunawatumia ujumbe; yule katika wawili hao atayetangulia ambaye basi tutamwacha mwingine. Wakawatumia ujumbe wawili hao na akatangulia kuja yule mtu anayefanya Lahd. Hivyo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akafanyiwa Lahd.”

 Ameipokea Ibn Maajah (01/472), at-Twahaawiy (04/45) na Ahmad (03/99).

Cheni ya wapokezi ni nzuri. Hivo ndivo alivosema al-Haafidhw katika “at-Takhiysw” (05/204).

Inayo shahidi mbili:

1- Kutoka kwa Ibn ´Abbaas.

Ameipokea Ibn Maajah (01/298), Ahmad (39, 3358), Ibn Sa´d (02/02/72) na al-Bayhaqiy (03/407).

2- Kutoka kwa ´Aaishah.

Ameipokea Ibn Maajah na Ibn Sa´d. Cheni zote wapokezi wote wawili ni dhaifu. Hayo yamesemwa na al-Haafidhw. Lakini ya kwanza katika mbili hizo inayo njia nyingine kwa tamko lisemalo:

“Kaburi la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliingia ndani al-´Abbaas, ´Aliy na al-Fadhwl. Bwana mmoja katika Answaar akalinganisha sawa Lahd yake. Bwana huyo ndiye ambaye alitengeneza ile mianandani ya wale mashahidi wa siku ya Badr.”

Ameipokea at-Twahaawiy katika “Mushkil al-Aathaar” (04/47), Ibn-ul-Jaaruud (268) na Ibn Hibbaan (2161) kwa cheni ya wapokezi Swahiyh. Ibn ´Abbaas ana Hadiyth nyingine kuhusu mwanandani kutoka katika maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ambayo yatakuja baada ya Hadiyth. Shahidi ya Hadiyth ya ´Aliy itakuja katika masuala ya 97, uk. 147.

Ya pili: ´Aamir bin Sa´d bin Abiy Waqqaas amepokea kutoka kutoka kwa baba yake ambaye amesema:

“Nifanyieni mimi Lahd na nizibieni juu yangu matofali kama alivofanyiwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).”

Ameipokea Muslim (02/61), an-Nasaa´iy (01/283), Ibn Maajah (01/471), at-Twahaawiy katika “al-Mushkil” (04/46), al-Bayhaqiy na Ahmad (1489, 1601, 1602).

Ya tatu: Ibn ´Abbaas amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

Lahd ni kwa ajili yetu na Shaqq ni kwa ajili ya wengine.”

Ameipokea Abu Daawuud (02/69), an-Nasaa´iy (01/283), at-Tirmidhiy (02/152), Ibn Maajah (4711), at-Twahaawiy (04/48) na al-Bayhaqiy (03/408) kwa cheni ya wapokezi dhaifu. Hayo yamesemwa na al-Haafidhw (05/203). Lakini ni Swahiyh kwa mujibu wa Ibn-us-Sakan.

Pengine amefanya hivo kutokana na Hadiyth zengine zinazoitolea ushahidi na njia zake ambazo miongoni mwazo ni zifuatazo:

Kutoka kwa Jariyr ambayo ameirufaisha kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mfano wake.

Ameipokea Ibn Maaajah, at-Twahaawiy, al-Bayhaqiy, at-Twayaalisiy (669), Ahmad (04/357, 359, 362) kutoka kwa ´Uthmaan bin ´Umayr bin Abiyl-Yaqdhwaan kutoka kwa Zaadhaan ambaye amepokea kutoka kwake.

´Uthmaan huyu ni mnyonge. Hayo yamesemwa na al-Haafidhw. Lakini at-Twahaawiy ameipokea katika njia nyingine na Ahmad kutoka njia mbili zengine. Njia hizi nne za Hadiyth hii zinapeana nguvu. Zikiongezwa juu ya Hadiyth ya Ibn ´Abbaas basi inapata nguvu kutokana na unyonge wake na inahama kwenda katika ngazi ya uzuri, bali Swahiyh.

an-Nawawiy amesema katika “al-Majmuu´” (05/287):

“Wanachuoni wameafikiana kwamba kuzika katika Lahd na Shaqq yote mawili yanafaa. Lakini ardhi ikiwa ngumu na udongo wake haubomoki, basi Lahd ndio bora zaidi kutokana na dalili zilizotangulia. Na ikiwa ardhi yake ni nyepesi inabomoka basi Shaqq ndio bora zaidi.”

[1] Lahd.

[2] Shaqq.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 182-184
  • Imechapishwa: 21/02/2022