94. al-´Ayyaashiy upotoshaji wake wa tano wa an-Nisaa´

al-´Ayyaashiy amesema alipokuwa akifasiri Aayah:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَطِيعُوا اللَّـهَ وَأَطِيعُوا الرَّسُولَ وَأُولِي الْأَمْرِ مِنكُمْ ۖ فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ إِن كُنتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّـهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۚ ذَٰلِكَ خَيْرٌ وَأَحْسَنُ تَأْوِيلًا

“Enyi walioamini! Mtiini Allaah na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi; mkizozana juu ya jambo, basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume mkiwa mnamuamini Allaah na siku ya Mwisho. Hivyo ni bora na matokeo mazuri kabisa.”[1]

Imewakusanya waumini mpaka siku ya Qiyaamah ya kwamba wanatakiwa kumtii Allaah, Mtume na wale wenye madaraka katika nyinyi. Anamaanisha sisi pekee. Uhakika wa mambo Aayah imeteremshwa namna hii:

فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللّهِ وَالرَّسُولِ وَأُوْلِي الأَمْرِ مِنكُمْ

“Mkizozana juu ya jambo, basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume na kwa wale walioshika madaraka katika nyinyi.”

Ni vipi itawezekana akawaamrisha watu wawatii wale walioshika madaraka katika wao lakini wasirudi kwao wakati wa kuzozana?”[2]

Aayah:

فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللَّـهِ وَالرَّسُولِ

“… mkizozana juu ya jambo, basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume… “

inawahusu waumini wote wakiwemo wale walioshika madaraka. Ni wajibu kuyarudisha kwa Allaah na kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam),  bi maana katika Kitabu cha Allaah na Sunnah za Mtume Wake Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Anakuja huyu Baatwiniy na wasapoti wake wanaoifanyia istihzai Qur-aan na walio na ujasiri katika kuipotosha na kuibadilisha na wanasema kuwa imeteremshwa namna hii:

فَإِن تَنَازَعْتُمْ فِي شَيْءٍ فَرُدُّوهُ إِلَى اللّهِ وَالرَّسُولِ وَأُوْلِي الأَمْرِ مِنكُمْ

“Mkizozana juu ya jambo, basi lirudisheni kwa Allaah na Mtume na kwa wale walioshika madaraka katika nyinyi.

[1] 04:59

[2] Tafsiyr al-´Ayyaashiy (1/247).

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Intisaar li Kitaab-il-´Aziyz al-Jabbaar, uk. 142
  • Imechapishwa: 23/11/2017