91. Dhikr wakati wa kufanya haja chooni na wakati wa jimaa

Ama kuhusu kufanya Dhikr wakati wa kujamiiana au wakati kukidha haja, hapana shaka ya kwamba haichukizwi kufanya ndani ya moyo, kwa kuwa moyo hauwezi kuepukana na kumdhukuru Yule anayempenda zaidi. Ikiwa moyo utaamrishwa kumsahau Yeye, basi hilo lingekuwa jambo lisilowezekana. Kama alivyosema mshairi:

Wanataka moyo usahau upendo wenu –

lakini umbile linakataa kutii mtoa amri

kuhusu kufanya Dhikr ya ulimi katika hali hiyo si katika mambo tuliyowekewa katika Shari´ah, Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakupendeza kwetu kufanya hivo na wala haikupokewa kutoka kwa Swahabah (Radhiya Allaahu ´anh) yeyote.

  • Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 163
  • Imechapishwa: 03/09/2025