Maana ya Bid´ah ni kuvumbua kitu pasi na kuwa na mfano wake hapo kabla. Amesema (Ta´ala):

بَدِيعُ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ

“Mwanzilishi wa mbingu na ardhi.”[1]

Bi maana aliyevianzisha pasi na mfano wake hapo kabla. Amesema (Ta´ala):

قُلْ مَا كُنتُ بِدْعًا مِّنَ الرُّسُلِ

“Sema: “Mimi sikuwa jambo jipya lilozuka katika Mitume.”[2]

Bi maana mimi sikuwa wa kwanza kuja na ujumbe kutoka kwa Allaah kwenda kwa waja. Bali wamenitangulia Mitume wengi. Inasemwa “fulani amevumbua uzushi” bi maana ameanzisha njia ambayo hakutanguliwa. Bid´ah zimegawanyika mafungu mawili:

Ya kwanza: Kuvumbua katika mambo ya kawaida. Kama mfano wa kuvumbua uvumbuzi wa kisasa. Haya yanajuzu. Kwa sababu kimsingi katika mambo ya kiada ni uhalali.

Ya pili: Kuvumbua katika dini. Kitendo hichi ni haramu. Kwa sababu kimsingi ni kukomeka. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Atakayezua katika amri yetu hii yale yasiyokuwemo atarudishiwa mwenyewe.”[3]

 Katika upokezi mwingine imekuja:

“Mwenye kufanya kitendo kisichoafikiana na amri yetu basi atarudishiwa mwenyewe.”[4]

[1] 02:117

[2] 46:09

[3] al-Bukhaariy (2550) na Muslim (1718).

[4] Muslim (4468).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ´Aqiydat-ut-Tawhiyd, uk. 167-169
  • Imechapishwa: 30/06/2020