44 – Dhikr ni kichwa cha shukurani. Hakumtaja Allaah (Ta´ala) yule ambaye hakumshukuru al-Bayhaqiy amesimulia kutoka kwa Zayd bin Aslam, ambaye ameeleza ya kwamba Muusa (‘alayhis-salaam) amesema:

”Ee Mola wangu! Hakika umenineemesha sana, basi niongoze juu ya jinsi ya kukushukuru kwa wingi.” Akasema: ”Nitaje kwa wingi. Ukinitaja kwa wingi basi umenishukuru kwa wingi, na ukinisahau basi umenikufuru.”[1]

Katika kitabu hichohicho al-Bayhaqiy amesimulia kutoka kwa ´Abdullaah bin Salaam (Radhiya Allaahu ´anh), aliyeeleza ya kwamba Muusa (‘alayhis-Salaam) amesema:

”Ee Mola wangu! Ni shukurani gani inayokupasa?” Allaah (Ta´ala) akamfunulia wahy: ”Ya kwamba moyo wako usiache kuwa na unyevu kwa kunitaja.” Akasema: ”Ee Mola, hakika inatokea wakati mwingine nakuwa katika hali ninayokutukuza zaidi kutokana na mimi kukutaja?” Akasema: ”Ni ipi hiyo?” Akasema: ”Nikiwa katika janaba, nikiwa chooni au nikikojoa.” Akasema: ”Hata hivyo.” Akasema: ”Ee Mola wangu, niseme nini?” Akasema: ”Sema: ”Umetakasika kutokana na mapungufu, na himdi zote njema ni Zako. Niepushe na madhara. ”Umetakasika kutokana na mapungufu, na imdi zote njema ni Zako. Nilinde kutokana na madhara.”[2]

´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akimtaja Allaah (Ta´ala) katika hali zake zote.”[3]

Hakubagua hali yoyote miongoni mwa hali zake. Hili linafahamisha ya kwamba alikuwa akimdhukuru Mola wake (Ta´ala) akiwa katika hali ya twahara na janaba. Ama akiwa katika hali ya kukojoa au kujisaidia hakuna aliyemuona akieleza hali hiyo. Lakini amewasunishia ummah wake Adhkaar kabla ya kuingia chooni na baada ya kutoka, jambo linalojulisha kutilia umuhimu mkubwa Dhikr na kwamba haiachwi hata kabla ya kukidhi haja na baada yake. Kadhalika amewasunishia ummah wake kufanya Dhikr, na kwamba mtu aseme:

”Mmoja wenu anapotaka kufanya jimaa na mke wake, basi na aseme:

بسم الله اللهم جَنِّبْنَا الشَّيْطَانَ وَجَنِّبِ الشَّيْطَانَ مَا رَزَقْتَنَا

”Kwa jina la Allaah! Ee Allaah! Tulinde na shaytwaan na kilinde na shaytwaan kile ulichoturuzuku.”[4]

[1] Shu´b-ul-Iymaan (2/574) na (8/368).

[2] Shu´b-ul-Iymaan (2/591).

[3] Muslim (373).

[4] al-Bukhaariy (141, 3271, 3283 na 6388) na Muslim (1434).

  • Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 161-162
  • Imechapishwa: 03/09/2025