Inafaa kwake [mwanaume] kumwangalia [mwanamke] kwa kujiiba pasina yeye kujua. Jaabir (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Nilimchumbia mwanamke. Nilikuwa nikijificha ili niangalie yale yatayonivutia kuweza kumuoa. Hivyo nikawa nimemuoa.”[1]
Muhammad bin Maslamah (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Nilimchumbia mwanamke. Nilipanda juu ya mti wa mtende na kujificha ili niweze kumtazama.”[2]
Wakati walipomuuliza ni vipi anaweza kufanya kitu kama hicho wakati yeye ni Swahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Vipi anaweza kujificha kwa ajili ya mwanamke na kumwangalia pasina yeye kujua? Kwa vile yeye alikuwa ni Swahabah wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Akasema:
“Nilimsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema: “Allaah Akimfanya mtu kutaka kumchumbia mwanamke hakuna ubaya akamwangalia.”[3]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mmoja wenu akimchumbia mwanamke hakuna neno akamwangalia pasina yeye kujua ikiwa kama anamwangalia ili amchumbie.”[4]
Sharti hii ni muhimu. Amesema:
“… ikiwa kama anamwangalia ili amchumbie.”
Haipasi kwake kumwangalia ili kujifurahisha, kupata uzowefu wala kustarehe. Anatakiwa awe mkweli na mwenye maazimio ya kweli ya kutaka kumchumbia. La sivyo ni haramu kwake kumwangalia hata kama atasema kuwa anataka kumchumbia. Sharti ya kumwangalia mwanamke ni Allaah, ambaye Anajua kila kile ambacho macho yanaangalia na yenye kufichwa na vifua, Ajue ya kwamba kweli unataka kumchumbia.
[1] Abu Daawuud (2082). Nzuri kwa mujibu wa al-Albaaniy i ”al-Irwaa’” (1791).Tazama ”as-Swahiyhah” (99).
[2] Ibn Maajah (1864). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”as-Swahiyhah” (98).
[3] Ibn Maajah (1864) na Ahmad (3/493). Tazama ”as-Swahiyhah” (98) ya al-Albaaniy.
[4] Ahmad (5/424) na at-Twahaawiy katika ”Sharh Ma´aaniy al-Aathaar” (3/3959). Swahiyh kwa mujibhu wa al-Albaaniy katika ”as-Swahiyhah” (97).
- Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliym ar-Ruhayliy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Haqq-uz-Zawjayn, uk. 16-17
- Imechapishwa: 24/03/2017

Mhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliym ar-Ruhayliy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Haqq-uz-Zawjayn, uk. 16-17
Imechapishwa: 24/03/2017
https://firqatunnajia.com/9-kumtazama-mwanamke-kwa-kujiiba-katika-mnasaba-wa-posa/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)