Leo wamekuwa wengi wanaoichukia Sunnah iliyothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pale inapopingana na matamanio yao na yale wanayoyapenda. Miongoni mwa hayo ni masuala ya mu´amala kama vile ribaa iliyoenea kwa watu hii leo. Unapowaambia watu hii ni ribaa na kwamba Allaah na Mtume wameharamisha ribaa, basi utawaona ni wenye kuchukizwa na hilo. Hata kama hawayasemi hayo wazi… baadhi yao wanasema waziwazi. Wanachukia kuyasikia hayo na wanasema kwamba watu wote leo hii wanafanya hivo, huu ni uchumi wa ulimwengu, nyinyi mnakwenda kinyume na ulimwengu. Huku ni kuritadi kutoka katika Uislamu. Akiyachukia maandiko yanayoharamisha ribaa, kamari, nyamafu, mu´amala unaokwenda kinyume na dalili, kukipatikana katika nafsi yake chuki juu ya hayo, basi hakika Allaah anayaporomosha matendo yake japokuwa hatoongea, japokuwa atayafanya kiuinje. Khatari ni kubwa. Ni wajibu kwa muislamu aichunge nafsi yake, auhifadhi ulimi wake na atembee pamoja na haki popote itakapoenda. Asitembee pamoja na matamanio na shahawa zake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 116-117
  • Imechapishwa: 27/11/2018