43 – Hakika Dhikr ni sawa na kuwakomboa watumwa, ni sawa na kutoa mali na ni sawa na kubeba silaha katika njia ya Allaah (´Azza wa Jall). Pia Dhikr ni sawa na kupigana kwa upanga katika njia ya Allaah (´Azza wa Jall). Kama inavosema Hadiyth:
“Mwenye kusema:
لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌم
“Hapana mwabudiwa wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee hana na mshirika. Ufalme Wake na himdi Zake na Yeye juu ya kila kitu ni Muweza.”
mara mia kwa siku, basi analingana na aliyeacha watumwa kumi, ataandikiwa thawabu mia moja, atafutiwa makosa mia moja, atakingwa na shaytwaan katika siku hiyo mpaka ifike jioni. Hakuna mtu ambaye atakuja na kitu bora zaidi kuliko alichofanya isipokuwa mtu ambaye amefanya zaidi kuliko yeye. Mwenye kusema:
سبحان الله وبحمده
“Allaah ametakasika kutokana na mapungufu na himdi zote njema ni Zake.”
mara mia katika siku, basi dhambi zake zitafutwa hata kama zingekuwa kama povu la bahari.”[1]
Ibn Abiyd-Dunyaa amepokea kutoka kwa al-A´mash, kutoka kwa Saalim bin Abiyl-Ja´d, ambaye ameeleza:
”Kulisemwa kuambiwa Abud-Dardaa´ (Radhiya Allaahu ´anh) kuwa kuna bwana mmoja amekomboa watu mia, ambapo akasema: “Watu mia kutoka katika mali ya mtu mmoja ni nyingi, lakini bora zaidi ya hilo ni imani yenye kudumu, iliyoshikamana usiku na mchana, na bora kwamba ulimi usiache kuwa na unyevu wa kumtaja Allaah.”
Ibn Mas´uud (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:
“Kumtukuza Allaah (Ta´ala) mara nyingi kunapendeza zaidi kwangu kuliko kutoa idadi yake kwa dinari katika njia ya Allaah (´Azza wa Jall).”
Siku moja ´Abdullaah bin ´Amr na ´Abdullaah bin Mas´uud walikaa pamoja. Ibn Mas´uud akasema:
”Kusema:
سُبْحَانَ اللَّهِ والْحَمْدُ لِلَّهِ وَلَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَاللَّهُ أَكْبَرُ
”Allaah ametakasika kutokana na mapungufu. Himdi zote njema anastahiki Allaah. Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah. Allaah ni mkubwa.”
kunapendeza zaidi kwangu kuliko kutoa idadi yake kwa dinari katika njia ya Allaah.” Ndipo ´Abdullaah bin ´Amr:
“Inanipendeza zaidi kwangu kumtoa mnyama katika njia ya Allaah (´Azza wa Jall).”
Tumeshatangulia kutaja Hadiyth Abud-Dardaa´ ambaye ameeleza ya kwamba Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Je, nikuambieni kuhusu bora ya matendo yenu, yaliyo safi zaidi mbele ya Mola wenu, yenye kuinuliwa daraja zenu, bora kuliko kutoa dhahabu na fedha na bora kuliko kukutana na adui zenu na kuwakatakata shingo zao nao wakakatakata shingo zenu?” Wakasema: “Ndio, ee Mtume wa Allaah.” Akasema: ”Mtajeni Allaah (´Azza wa Jall).”[2]
Ameipokea Ibn Maajah, at-Tirmidhiy na al-Haakim, ambaye amesahihisha cheni yake ya wapokezi.
[1] al-Bukhaariy (3293 na 6403) na Muslim (2691).
[2] Ahmad (7/367-368). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika “Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (1493).
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 159-161
- Imechapishwa: 03/09/2025

Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 159-161
Imechapishwa: 03/09/2025
https://firqatunnajia.com/89-bora-kuliko-kutoa-swadaqah-na-kuacha-huru-watumwa/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket