84 – Imekuja kwa al-Bukhaariy na Muslim ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwaombea du´aa watu akasema:

أَكَلَ طعامَكُمُ الأبرارُ ، وأفطرَ عندَكُمُ الصَّائمونَ ، وصلَّت عليكُمُ الملائِكَةُ، وذكرَكُم اللَّهُ فيمَن عندَهُ

”Wale chakula chenu waja wema. Wafuturu kwenu wafungaji. Malaika wawaombeeni msamaha. Allaah akutajeni mbele ya wale walioko Kwake.”

Allaah (Ta´ala) amesema:

إِنَّ الَّذِينَ عِندَ رَبِّكَ لَا يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِهِ وَيُسَبِّحُونَهُ وَلَهُ يَسْجُدُونَ

“Hakika wale walioko kwa Mola wako hawatakabari kufanya ‘ibaadah Yake na wanamsabihi na Kwake pekee wanasujudu.”[1]

وَلَهُ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ ۚ وَمَنْ عِندَهُ لَا يَسْتَكْبِرُونَ عَنْ عِبَادَتِهِ وَلَا يَسْتَحْسِرُونَ يُسَبِّحُونَ اللَّيْلَ وَالنَّهَارَ لَا يَفْتُرُونَ

“Na ni Vyake pekee vyote vilivyomo katika mbingu na ardhi na wale walio Kwake hawatakabari na ‘ibaadah Yake na wala hawachoki. Wanasabihi usiku na mchana wala hawazembei.”[2]

Muslim amepokea kwamba Abu Hurayrah amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Aadam na Muusa walihojiana mbele ya Mola wao… ”[3]

[1] 7:206

[2] 21:19-20

[3] Hadiyth hii ni Swahiyh, lakini hakuna ziada iliopo mwishoni mwake:

و ذكركم الله فيمن عنده

”Allaah akutajeni mbele ya wale walioko Kwake.”

Haipo kabisa kwa al-Bukhaariy na Muslim, kama nilivyozindua hilo katika ”Aadaab-uz-Zifaaf”, na huko utapata uhakiki wake wa kipekee. Hata hivyo ziada iliyotajwa imekuja katika Hadiyth nyingine:

“Hawatokusanyika watu katika nyumba miongoni mwa nyumba za Allaah wakikisoma Kitabu cha Allaah na wakikidurusu kati yao, isipokuwa wanateremkiwa na utulivu, rehema huwafunika na Malaika huwazunguka na Allaah huwataja kwa wale walioko Kwake.”

Ameipokea Muslim, Ahmad na wengineo na imetajwa katika kitabu changu “Swahiyh Sunan Abiy Daawuud” (1308). Ni kana kwamba mtunzi amezichanganya Hadiyth hizo mbili.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-´Uluww lil-´Aliy al-Ghaffaar, uk. 107
  • Imechapishwa: 03/07/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy