41 – Hakika Dhikr ni kama mti unaochipua maarifa na hali njema ambazo wenye kutafuta wamezihimiza. Hakuna njia ya kupata matunda yake isipokuwa kupitia mti wa Dhikr. Kila inapokuwa Dhikr ni kubwa zaidi na mizizi yake imesimama imara matunda yake huwa bora zaidi. Dhikr huchipua ngazi zote za kimaadili, kuanzia kwenye kuzinduka mpaka kwenye upwekeshaji. Dhikr ni msingi wa kila daraja na ndio msingi wake ambao daraja hilo hujengwa juu yake, kama ukuta unavyobeba dari. Hakika mja asipozinduka hawezi kuvuka hatua muhimu za safari, na wala hawezi kuamka isipokuwa kwa utajo wa Allaah. Kwa hiyo ughafilikaji ni usingizi wa moyo au kifo chake.
42 – Hakika Dhikr humfanya mja kuwa karibu na mwenye kumdhukuru na mwenye kumdhukuru yuko naye. Huu ni upamoja maalum na si upamoja wa ujuzi na uzungukaji wa jumla. Huu ni upamoja wa ukaribu, ulinzi, mapenzi, nusura na tawfiyq. Kama alivyosema (Ta´ala):
إِنَّ اللَّـهَ مَعَ الَّذِينَ اتَّقَوا وَّالَّذِينَ هُم مُّحْسِنُونَ
“Hakika Allaah yupamoja na wenye kumcha na wale watendao wema.”[1]
وَالَّذِينَ جَاهَدُوا فِينَا لَنَهْدِيَنَّهُمْ سُبُلَنَا ۚ وَإِنَّ اللَّـهَ لَمَعَ الْمُحْسِنِينَ
“Na wale waliofanya juhudi kwa ajili Yetu, bila shaka Tutawaongoza njia Zetu. Hakika Allaah yupamoja na wafanyao wema.”[2]
كَم مِّن فِئَةٍ قَلِيلَةٍ غَلَبَتْ فِئَةً كَثِيرَةً بِإِذْنِ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ مَعَ الصَّابِرِينَ
“Makundi mangapi machache yameshinda makundi mengi kwa idhini ya Allaah? Na Allaah yupamoja na wenye kusubiri.”[3]
إِذْ يَقُولُ لِصَاحِبِهِ لَا تَحْزَنْ إِنَّ اللَّـهَ مَعَنَا
“Alipomwambia swahiba yake: “Usihuzunike – hakika Allaah yupamoja nasi!”[4]
Yule mwenye kufanya Dhikr analo fungu kubwa la upamoja huu. Imekuja katika Hadiyth ya kiungu:
”Allaah amesema: ”Mimi niko pamoja na mja Wangu maadamu ananitaja na midomo yake inatikisa kwa ajili Yangu.”[5]
Imekuja katika masimulizi mengine:
“Wale watu wenye kunitaja ni watu wa kukaa pamoja na Mimi. Wale watu wenye kunishukuru ni watu wenye kunitembelea. Wale watu wenye kunitii ni watu wa kuheshimiwa Kwangu. Wale watu wenye kuniasi siwakatishi tamaa na rehema Yangu. Wakitubu, basi Mimi ni mwenye kuwapenda, kwa sababu Mimi ninawapenda wenye kutubu na nawapenda wenye kujitakasa. Na wasipotubu, basi Mimi ni daktari wao; Ninawapa mitihani ya misiba ili niwatakase kutokana na makosa.”
[1] 16:128
[2] 29:69
[3] 2:249
[4] 9:40
[5] Ibn Maajah (3792), Ahmad (3/820-821), Ibn Hibbaan (815), al-Bukhaariy katika “Khalqu Af´aal-il-´Ibaad” (450), al-Haakim (1/496), ambaye amesahihisha cheni ya wapokezi wake na adh-Dhahabiy akaafikiana naye.
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 157-158
- Imechapishwa: 02/09/2025

Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 157-158
Imechapishwa: 02/09/2025
https://firqatunnajia.com/87-hapa-ndipo-huzindukana/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket