86. Uharamu kwa anayefanya I´tikaaf kufanya tendo la ndoa na vitangulizi vyake

Ni haramu kwa anayefanya I´tikaaf kufanya tendo la ndoa, vitangulizi vyake kukiwemo kubusu na kupapasa kwa matamanio. Amesema (Ta´ala):

وَلَا تُبَاشِرُوهُنَّ وَأَنتُمْ عَاكِفُونَ فِي الْمَسَاجِدِ

“Na wala msichanganyike nao hali ya kuwa nyinyi ni wenye kukaa I’tikaaf  misikitini.”[1]

Hapana vibaya kutoka msikitini ikiwa atatoa baadhi ya sehemu ya mwili wake. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesimulia:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akitoa kichwa chake nje ya msikiti ilihali anafanya I´tikaaf ambapo nikakiosha nami niko na hedhi.”

Ameipokea al-Bukhaariy.

Imepokelewa katika upokezi mwingine:

“Alikuwa akichanua kichwa cha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ilihali yuko na hedhi na yeye yuko katika I´tikaaf msikitini na yeye ´Aaishah akiwa chumbani mwake ambapo anamnyooshea kichwa chake.”

[1] 02:187

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 157
  • Imechapishwa: 12/03/2024