39 – Dhikr hukusanya kilichotawanyika na hutawanya kilichokusanyika, hukaribisha kilicho mbali na hukiweka mbali kilicho karibu. Hukusanya kile kilichotawanyika kwa mja kama moyo wake, matamanio yake, mawazo yake na maamuzi yake. Adhabu kubwa ni katika kutawanyika kwake, kuchanganyikiwa kwake na kupotea kwake. Lakini maisha ya furaha na neema imo katika kuungana kwa moyo, nia hamu na azma yake.
Dhikr hutawanya yale yaliyokusanyika juu ya mja kama huzuni, dhiki, majonzi na majuto kwa kupitwa na matamanio na mahitaji yake. Na pia hutawanya madhambi yake, makosa yake na mizigo yake iliyomzonga mpaka yaanguke yote, yatoweke na kupotea.
Dhikr huwatawanya maadui waliomkusanyikia kumshambulia kutoka katika jeshi la shaytwaa. Ibliys daima hutuma vikosi dhidi yake. Kila ambavyo mja anakuwa mwenye nguvu zaidi, kufungamana na kumwelekea Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala), ndivyo inavyokuwa vikosi vinavyomshambulia vingi zaidi na vyenye nguvu zaidi kulingana na kiwango cha kheri na nia aliyonayo mja. Hapana njia ya kuyatawanya majeshi hayo isipokuwa kwa kudumu na Dhikr.
Kuhusu Dhikr kumkaribisha aliyekuwa mbali ni kwamba humkaribisha mja na Aakhirah ambayo shaytwaan na tamaa huwa wanataka kumfanya aiwe mbali. Hivyo mja huendelea kushughulika na Dhikr mpaka afikie hali kwamba ni kama ameshaingia Aakhirah na kuikuta. Wakati huo basi ulimwengu huwa ndogo machoni pake na Aakhirah huwa kubwa moyoni mwake.
Dhikr humuweka mbali na dunia ambayo ni karibu naye zaidi kuliko Aakhirah. Kwani pindi Aakhirah inavyokaribia moyoni mwake, basi dunia humuacha mbali. Kila Aakhirah inavyomkaribia kwa hatua, basi ulimwengu humtoka kwa hatua. Hakuna njia ya kuyafikia haya isipokuwa kwa kudumu katika Dhikr.
40 – Hakika Dhikr humwamsha moyo kutoka usingizini na humwamsha kutoka kwenye usingizi mzito. Moyo unapolala, hupitwa na faida na biashara ya kheri na huelemea kwenye khasara. Lakini unapozinduka na kufahamu kilichompita alipokuwa amelala, basi hujifunga mkanda, akaanza kuishi muda wake uliobaki na akijitahidi kurekebisha kile kilichompita. Huwezi kupata kuzinduka isipokuwa kwa Dhikri. Kwani upumbaaji ni usingizi mzito.
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 155-157
- Imechapishwa: 02/09/2025
39 – Dhikr hukusanya kilichotawanyika na hutawanya kilichokusanyika, hukaribisha kilicho mbali na hukiweka mbali kilicho karibu. Hukusanya kile kilichotawanyika kwa mja kama moyo wake, matamanio yake, mawazo yake na maamuzi yake. Adhabu kubwa ni katika kutawanyika kwake, kuchanganyikiwa kwake na kupotea kwake. Lakini maisha ya furaha na neema imo katika kuungana kwa moyo, nia hamu na azma yake.
Dhikr hutawanya yale yaliyokusanyika juu ya mja kama huzuni, dhiki, majonzi na majuto kwa kupitwa na matamanio na mahitaji yake. Na pia hutawanya madhambi yake, makosa yake na mizigo yake iliyomzonga mpaka yaanguke yote, yatoweke na kupotea.
Dhikr huwatawanya maadui waliomkusanyikia kumshambulia kutoka katika jeshi la shaytwaa. Ibliys daima hutuma vikosi dhidi yake. Kila ambavyo mja anakuwa mwenye nguvu zaidi, kufungamana na kumwelekea Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala), ndivyo inavyokuwa vikosi vinavyomshambulia vingi zaidi na vyenye nguvu zaidi kulingana na kiwango cha kheri na nia aliyonayo mja. Hapana njia ya kuyatawanya majeshi hayo isipokuwa kwa kudumu na Dhikr.
Kuhusu Dhikr kumkaribisha aliyekuwa mbali ni kwamba humkaribisha mja na Aakhirah ambayo shaytwaan na tamaa huwa wanataka kumfanya aiwe mbali. Hivyo mja huendelea kushughulika na Dhikr mpaka afikie hali kwamba ni kama ameshaingia Aakhirah na kuikuta. Wakati huo basi ulimwengu huwa ndogo machoni pake na Aakhirah huwa kubwa moyoni mwake.
Dhikr humuweka mbali na dunia ambayo ni karibu naye zaidi kuliko Aakhirah. Kwani pindi Aakhirah inavyokaribia moyoni mwake, basi dunia humuacha mbali. Kila Aakhirah inavyomkaribia kwa hatua, basi ulimwengu humtoka kwa hatua. Hakuna njia ya kuyafikia haya isipokuwa kwa kudumu katika Dhikr.
40 – Hakika Dhikr humwamsha moyo kutoka usingizini na humwamsha kutoka kwenye usingizi mzito. Moyo unapolala, hupitwa na faida na biashara ya kheri na huelemea kwenye khasara. Lakini unapozinduka na kufahamu kilichompita alipokuwa amelala, basi hujifunga mkanda, akaanza kuishi muda wake uliobaki na akijitahidi kurekebisha kile kilichompita. Huwezi kupata kuzinduka isipokuwa kwa Dhikri. Kwani upumbaaji ni usingizi mzito.
Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 155-157
Imechapishwa: 02/09/2025
https://firqatunnajia.com/86-hapo-ndipo-huanza-kuishi/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket