37 – Hakika Dhikr ndio kichwa cha misingi yote, njia ya wengi wa waliyochaguliwa na ni kitangazo cha uwalii. Hivyo basi atakayefunguliwa milango ya Dhikr basi amefunguliwa mlango wa kuingia kwa Allaah (´Azza wa Jall). Kwa hiyo ajitwaharisheni kisha aingie kwa Mola wake (´Azza wa Jall), naye atakuta hapo kila anachokitaka. Akimpata Mola wake (´Azza wa Jall), basi amepata kila kitu. Asipompata Mola wake (´Azza wa Jall), basi amekosa na kila kitu.

38 – Ndani ya moyo mna umasikini na mahitaji ambayo hayazibwi kabisa na kitu kingine chochote isipokuwa utajo wa Allaah (´Azza wa Jall). Hivyo ikawa Dhikr ndio nguo ya moyo kiasi kwamba moyo unakuwa ndio mwenye Dhikr kwa msingi na ulimi hufuata tu, basi hii ndio Dhikr inayoziba umasikini huo na huondosha uhitaji. Matokeo yake mwenye nayo anakuwa ni tajiri bila mali, mwenye heshima bila ukoo, mwenye haiba bila mamlaka. Lakini anapokuwa mwenye kughafilika na kumtaja Allaah (´Azza wa Jall), basi anakuwa kinyume na hivo; fakiri pamoja na wingi wa mali, dhalili pamoja na mamlaka, duni pamoja na wingi wa jamaa.

  • Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 155
  • Imechapishwa: 02/09/2025