85. Sampuli za watu wanaochukia yale aliyoteremsha Allaah na tofauti ya wao na waumini wa kweli

Wale wanaochukia yale aliyoteremsha Allaah (´Azza wa Jall) wamegawanyika makundi mawili:

Kundi la kwanza: Wale ambao kimsingi ni makafiri. Haya ndio maneno yao.

Kundi la pili: Wale ambao wanadai Uislamu, ambao ni wanafiki. Maneno yao yamekwishatangulia.

Kuhusu waumini hakika wao wanapenda yale yaliyokuja kutoka kwa Allaah na Mtume (Swalla Allaahu ´aalyhi wa sallam). Kwa ajili hiyo amesema (Ta´ala) kuhusu wao:

إِنَّمَا كَانَ قَوْلَ الْمُؤْمِنِينَ إِذَا دُعُوا إِلَى اللَّـهِ وَرَسُولِهِ لِيَحْكُمَ بَيْنَهُمْ أَن يَقُولُوا سَمِعْنَا وَأَطَعْنَاۚوَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ

“Hakika kauli ya waumini wa kweli wanapoitwa kwa Allaah na Mtume wake ili awahakumu kati yao, basi husema: “Tumesikia na Tumetii” – na hao ndio wenye kufaulu.” (an-Nuur 24:51)

Wanasema kuwa wamesikia na wametii kwa sababu wanampenda Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hawapati na wala hawahisi ndani ya nyoyo zao uzito wowote juu ya hukumu ya Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا

”Basi Naapa kwa Mola wako kwamba hawatoamini mpaka wakufanye wewe ni hakimu katika yale wanayozozana baina yao, kisha kusipatikane katika nyoyo zao uzito wowote katika uliyohukumu na wajisalimishe hali ya kujisalimisha kikweli” (an-Nisaa´ 04:65)

Hawaoni na wala hawahisi uzito wowote kwenye nafsi zao. Hawaoni kigugumizi kujisalimisha kwa uinje. Bali ni wenye kujisalimisha kwa uinje na kwa undani. Wanaipenda hukumu ya Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa uinje na kwa undani:

فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا

”Basi Naapa kwa Mola wako kwamba hawatoamini mpaka wakufanye wewe ni hakimu katika yale wanayozozana baina yao, kisha kusipatikane katika nyoyo zao uzito wowote katika uliyohukumu na wajisalimishe hali ya kujisalimisha kikweli” (an-Nisaa´ 04:65)

Bi maana hawapati na hawahisi uzito wowote katika nafsi na nyoyo zao. hawawi na uzito katika nafsi zao na nyoyo zao, haitoshi kunyenyekea kwa uinje, isipokuwa wanajisalimisha kwa nje na kwa ndani na wanapenda hukumu ya Allaah  na hukumu ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) nje na ndani. Hawapingani na hukumu ya Allaah na hukumu ya Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa kuwa wanajua kuwa ndio ya haki na adilifu na kwamba mwisho wake ni wenye kusifiwa. Hawatangulizi chochote kabla ya hukumu ya Allaah na ya Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), japokuwa ni chenye kwenda kinyume na matamanio yao na matakwa yao, wanaacha maoni yao na matakwa yao na wanakubali hukumu ya Allaah na ya Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa sababu anajua kheri iliyomo ndani yake duniani na Aakhirah. Hawa ndio waumini. Inapowafikia hukumu ya Allaah na ya Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), basi hawataki badala yake kwa hali yoyote ile. Vilevile hawaipi chanzo wala hukumu yoyote ile kipaumbele mbele ya Qur-aan na Sunnah. Hizi ndizo sifa za waumini. Kwa ajili hiyo ndio maana utawaona ni wenye kupupia na ni wenye kukimbilia kujifunza Qur-aan na Sunnah. Wako tayari kuvumilia tabu na shida kwa kuwa wanapenda Qur-aan na Sunnah. Vitu hivi viwili kwao ni vyenye kupendwa zaidi kuliko vyakula na vinywaji. Hayo ni tofauti na wanafiki. Wao wanakimbia mbali na Qur-aan na Sunnah au wanaisoma kwa ndimi zao tu na huku wanazimbia Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Amesema (Ta´ala):

رَأَيْتَ الْمُنَافِقِينَ يَصُدُّونَ عَنكَ صُدُودًا

”… utawaona wanafiki wanakugeuka kikwelikweli.” (an-Nisaa´ 04:61)

وَإِذَا قِيلَ لَهُمْ تَعَالَوْا يَسْتَغْفِرْ لَكُمْ رَسُولُ اللَّـهِ لَوَّوْا رُءُوسَهُمْ وَرَأَيْتَهُمْ يَصُدُّونَ وَهُم مُّسْتَكْبِرُونَ

”Wanapoambiwa: “Njooni ili Mtume wa Allaah akuombeeni msamaha”, basi hupindisha vichwa vyao na utawaona wanakwepa nao ni wenye kutakabari.” (al-Munaafiquun 63:05)

Hii ni alama ya kwamba wanaichukia Qur-aan cha Allaah na Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Nawaaqidh-il-Islaam, uk. 113-114
  • Imechapishwa: 22/11/2018