Yeye ndiye wa Kwanza; ambaye hakuna kitu kabla Yake. Yeye ndiye Mwisho; ambaye hakuna kitu baada Yake. Yeye ni wa dhahiri; ambaye hakuna kitu juu Yake. Aliyefichikana; ambaye hakuna chochote kilichojifika Kwake. Aliyebarikika na kutukuka. Ndiye anayestahiki zaidi kutajwa. Anayestahiki zaidi kuabudiwa. Anayestahiki zaidi kushukuriwa. Anayestahiki zaidi kusifiwa. Yeye ndiye wa kwanza zaidi kuombwa msaada. Yeye ndiye mwenye huruma zaidi kati ya wanaomiliki. Yeye ndiye mkarimu zaidi aliyeombwa. Yeye ndiye mwenye kusamehe zaidi mwenye uwezo. Yeye ndiye mkarimu zaidi anayekusudiwa. Yeye ndiye mwenye haki zaidi anayelipiza.
Subira Yake ipo baada ya ujuzi Wake. Msamaha Wake licha ya uwezo Wake. Msamaha Wake licha ya uwezo Wake. Kuzuilia Kwake baada ya hekima Yake. Mapenzi Yake kutokana na wema na rehema Zake.
Hakuna haki ya lazima juu Yake kwa waja – sivyo kabisa
Wala jitihada yoyote haipotei mbele Yake
Wakiadhibiwa, basi ni kwa uadilifu Wake
Wakineemeshwa, basi ni kwa fadhilah Zake – Naye ni Mkarimu, Mwenye wasaa
Yeye ni Mfalme asiye na mshirika. Yeye ni wa pekee asiye na mwenza. Yeye ni Mkwasi asiye na msaidizi. Yeye ni Mwenye kukusudiwa katika mambo yote asiye na mwana wala mke. Yeye Yuko juu asiye na anayefanana wala mwenye jina kama Lake. Kila kitu kitaangamia isipokuwa uso Wake. Kila ufalme utapotea isipokuwa ufalme Wake. Kila kivuli kitaondoka isipokuwa kivuli Chake. Kila fadhilah itakatika isipokuwa fadhilah Yake. Hakutiiwa na akalipa thawabu, huasiwa akapuulizia mbali na kusamehe. Kila adhabu Yake ni uadilifu. Kila neema Yake ni fadhilah. Yuko karibu zaidi wa kushuhudia na wa karibu zaidi wa kuhifadhi – yuko karibu zaidi na nafsi zao wenyewe. Yeye hushikilia kufuli zao na kuandika matendo yao. Ameandika muda wa maisha. Mioyo iko wazi Kwake. Siri Kwake ziko wazi. Mambo yaliyofichika Kwake ni yenye kudhihiri. Utoaji Wake ni maneno na adhabu Yake ni maneno:
إِنَّمَا أَمْرُهُ إِذَا أَرَادَ شَيْئًا أَن يَقُولَ لَهُ كُن فَيَكُونُ
”Hakika si venginevyo amri Yake anapotaka chochote hukiambia: “Kuwa!” nacho huwa.”[1]
Basi nuru za sifa hizi zinapong’ara ndani ya moyo, nuru nyingine yoyote huzimika mbele yake. Nyuma ya hayo yapo yasiyowahi kuingia akilini wala hayafikiki kwa maneno yoyote. Tunachotaka kusema ni kwamba Dhikr huung´arisha moyo, uso na viungo vya mwili. Ndio nuru ya mja katika ulimwengu wake, ndani ya kaburi na siku ya Qiyaamah.
Kwa kadiri ya nuru ya imani ndani ya moyo wa mja ndipo vinavyotiririka vitendo vyake na maneno yake, navyo vikiwa na nuru na hoja. Mpaka muumini hufikia kuwa nuru ya matendo yake yanapopanda juu kwa Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) huwa kama nuru ya jua. Ndivyo pia inavyokuwa nuru ya roho yake anapomrejea Allaah (´Azza wa Jall). Ndivyo inavyokuwa nuru ya uso wake siku ya Qiyaamah.
[1] 36:82
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 153-154
- Imechapishwa: 02/09/2025

Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 153-154
Imechapishwa: 02/09/2025
https://firqatunnajia.com/84-nuru-yako-duniani-ndani-ya-kaburi-na-aakhirah/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket