84. Hoja juu ya kwamba maiti ananufaika kwa matendo ya wengine

Katika mambo yanayoweza kuwa na umuhimu kuyataja katika mnasaba wa thawabu kumnufaisha yule maiti ni kuwa imependekezwa kuzikwa pembezoni na watu wema ili mtu aweze kupata sehemu katika baraka zao. Imaam Ahamd amesema kuwa maiti huudhika kwa yale madhambi yanayofanywa pembezoni na kaburi lake.

Imepokelewa kuwa Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

“Chungeni kumzika maiti karibu na mtu muovu.”

´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

“Maiti huudhika ndani ya kaburi lake na kile chenye kumuudhi nyumbani kwake.”

Hata kama kuna udhaifu katika mapokezi haya mawili, kuna ishara juu ya suala lenyewe. Ikiwa maiti anaudhika kwa madhambi basi ana haki zaidi ya kunufaika kwa matendo ya kheri. Imesihi ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hakika maiti anaadhibiwa kwa familia yake kumlilia.”

Allaah (Ta´ala) ni Mwingi wa hekima na mwadilifu wa kuacha maiti akafikiwa na adhabu ya madhambi na si thawabu za tendo jema na Allaah ndiye anajua zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 184
  • Imechapishwa: 26/11/2016