Mioyo ya waja na maingiliano yao yako mkononi Mwake. Hatamu za mambo zimefungwa kwa hukumu na makadirio Yake. Ardhi yote itakuwa katika mshiko Wake siku ya Qiyaamah na mbingu zitakunjwa mkononi Mwake wa kuume. Atazikamata mbingu Zake zote kwa mkono Wake mtukufu na ardhi kwa mkono mwingine, kisha atazitingisha kisha atasema: Mimi ni Mfalme, Mimi ni Mfalme! Mimi ndiye niliyeianzisha dunia hii na haikuwa kitu – na Mimi ndiye nitakayerudisha kama nilivyoianza!
Hakuna dhambi kubwa inayomshinda kuisamehe wala haja inayoulizwa inayomshinda kuipatia. Lau wakazi wote wa mbingu Zake, wakazi wa ardhi Yake, wa mwanzo wa viumbe Vyake na wa mwisho wao, wa binadamu wao na wa majini wao wangekuwa juu ya moyo mchamungu zaidi wa mtu mmoja kati yao, basi hilo halingeongeza chochote katika ufalme Wake. Lau wa mwanzo wa viumbe Vyake na wa mwisho wao, wa binadamu wao na wa majini wao wangekuwa juu ya moyo mwovu zaidi wa mtu mmoja kati yao basi hilo halingepunguza chochote kutoka katika ufalme Wake. Lau wakazi wa mbingu Zake na wakazi wa ardhi Yake, wa binadamu wao na wa majini wao, walio hai wao na waliokufa wao, wa majimaji wao na wa makavu wao wangesimama mahali pamoja na kumuomba Naye akawapa kila mmoja wao kile alichoomba basi hilo halingepunguza chochote kutoka katika kilicho Kwake hata uzito wa chembe.
Lau miti yote ya ardhini – tangu ilipoumbwa hadi mwisho wa dunia – ingekuwa kalamu, na bahari nyuma yake bahari saba zinazoiunga mkono, kuwa wino zingeisha kalamu na wino ungeisha, lakini maneno ya Muumba (Tabaarak wa Ta´ala) yasingeisha. Vipi yawezekana maneno Yake yaishe ilihali hayana mwanzo wala mwisho? Viumbe ndio wenye mwanzo na mwisho. Basi wao wanastahiki zaidi kufa na kwisha. Vipi kiumbe kife bali kisichoumbwa kisiishe?
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 152-153
- Imechapishwa: 01/09/2025
Mioyo ya waja na maingiliano yao yako mkononi Mwake. Hatamu za mambo zimefungwa kwa hukumu na makadirio Yake. Ardhi yote itakuwa katika mshiko Wake siku ya Qiyaamah na mbingu zitakunjwa mkononi Mwake wa kuume. Atazikamata mbingu Zake zote kwa mkono Wake mtukufu na ardhi kwa mkono mwingine, kisha atazitingisha kisha atasema: Mimi ni Mfalme, Mimi ni Mfalme! Mimi ndiye niliyeianzisha dunia hii na haikuwa kitu – na Mimi ndiye nitakayerudisha kama nilivyoianza!
Hakuna dhambi kubwa inayomshinda kuisamehe wala haja inayoulizwa inayomshinda kuipatia. Lau wakazi wote wa mbingu Zake, wakazi wa ardhi Yake, wa mwanzo wa viumbe Vyake na wa mwisho wao, wa binadamu wao na wa majini wao wangekuwa juu ya moyo mchamungu zaidi wa mtu mmoja kati yao, basi hilo halingeongeza chochote katika ufalme Wake. Lau wa mwanzo wa viumbe Vyake na wa mwisho wao, wa binadamu wao na wa majini wao wangekuwa juu ya moyo mwovu zaidi wa mtu mmoja kati yao basi hilo halingepunguza chochote kutoka katika ufalme Wake. Lau wakazi wa mbingu Zake na wakazi wa ardhi Yake, wa binadamu wao na wa majini wao, walio hai wao na waliokufa wao, wa majimaji wao na wa makavu wao wangesimama mahali pamoja na kumuomba Naye akawapa kila mmoja wao kile alichoomba basi hilo halingepunguza chochote kutoka katika kilicho Kwake hata uzito wa chembe.
Lau miti yote ya ardhini – tangu ilipoumbwa hadi mwisho wa dunia – ingekuwa kalamu, na bahari nyuma yake bahari saba zinazoiunga mkono, kuwa wino zingeisha kalamu na wino ungeisha, lakini maneno ya Muumba (Tabaarak wa Ta´ala) yasingeisha. Vipi yawezekana maneno Yake yaishe ilihali hayana mwanzo wala mwisho? Viumbe ndio wenye mwanzo na mwisho. Basi wao wanastahiki zaidi kufa na kwisha. Vipi kiumbe kife bali kisichoumbwa kisiishe?
Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 152-153
Imechapishwa: 01/09/2025
https://firqatunnajia.com/83-ufalme-wa-mola-usioathiriwa/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket