83. Ni ipi hukumu ya kwenda katika jihaad pasi na idhini ya mtawala?

Swali 83: Ni ipi hukumu ya kwenda katika jihaad pasi na idhini ya mtawala? Kwani mpiganaji jihaad anasamehewa kwa lile tone la kwanza linalodondoka; je, anazingatiwa kuwa amekufa shahidi?

Jibu: Akienda kinyume na kumuasi mtawala na wazazi anazingatiwa ni mtenda dhambi[1].

[1] Katika hali hii na hali ya swali lililo kabla yake muislamu analazimika kupata ruhusa ya mtawala, kwa sababu amekula kiapo cha utiifu kwake. Ni vipi basi atatoka pasi na idhini yake? Imaam Abu Bakr Muhammad bin al-Waliyd at-Twartwushiy amesema:

”Tamiym ad-Daariy (Radhiya Allaahu ´anh) alisema kumwambia ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anh): ”Niache nilinganie kwa Allaah, nieleze visa na niwakumbushe watu.” ´Umar akasema: ”Hapana.” (Kitaab-ul-Hawaadith wal-Bid´ah, uk. 109)

Ikiwa Tamiym alimuomba ruhusa ´Umar (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ya kulingania na kukumbusha na akakataliwa, basi ruhusa kwa ajili ya kitu kingine kilicho chini ya hapo ina haki zaidi na ni muhimu zaidi. Hii leo baadhi ya wamehoji idhini ya mtawala kwa ajili ya Qunuut. Hili si jengine isipokuwa linathibitisha kuwa watu hawa wanawachezea shere wale wanaolingania kumtii mtawala katika yasiyokuwa maasi. Kwa sababu kwa kufanya hivo anapingana na Qur-aan, Sunnah na maafikiano. Endapo wangelikuwa na elimu na kumcha Allaah basi kamwe wasingelisema hivo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 209-210
  • Imechapishwa: 23/07/2024
  • taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy