Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:
Wanaitakidi maana ya maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Muumini kwa muumini mwenzake ni kama jengo; upande mmoja unaupa nguvu upande mwingine.”[1]
Halafu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akakutanisha baina ya vidole vyake viwili. Vilevile maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Mfano wa waumini katika kupendana kwao, kuhurumiana kwao na kuhisiana kwao ni kama mfano wa mwili mmoja. Wakati kiungo cha mwili kinapatwa na maumivu, basi mwili mzima unapatwa na homa na kukosa usingizi.”[2]
Wanaamrisha kuwa na subira wakati wa mitihani, kuwa na shukurani wakati wa raha na kuridhia wakati wa kipindi kizito. Wanalingania katika maadili mema na matendo mema na wanaamini maana ya maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Muumini mwenye imani kamilifu zaidi ni yule mwenye tabia nzuri zaidi.”[3]
Wanahimiza kumuunga yule aliyekukata, umpe yule aliyekunyima na umsamehe yule aliyekudhulumu. Wanaamrisha kuwatendea wema wazazi wawili, kuwaunga ndugu, kuwatendea wema majirani, kuwafanyia wema mayatima na masikini na wasafiri na kuwafanyia upole watumwa. Sambamba na hayo wanakataza majivuno, kiburi, ukandamizaji na unyanyasaji kwa viumbe, ni mamoja iwe kwa haki au pasi na haki.
Wanaamrisha kuwa na maadili mema na wanakataza maadili mabaya. Na katika kila wanayoyasema na kuyafanya – katika haya na mengineyo – wanafuata Qur-aan na Sunnah. Njia yao ni dini ya Uislamu ambayo Allaah amemtumiliza kwayo Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini alipokhabarisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ya kwamba ummah wake utagawanyika mapote sabini na tatu na yote yataingia Motoni isipokuwa moja tu; nalo ni mkusanyiko[4].
Imekuja katika Hadiyth nyingine kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba amesema:
“Ni wale ambao watakuwemo kwa mfano wa yale niliyomo mimi hii leo na Maswahabah zangu.”[5]
wamekuwa wale wenye kushikamana barabara na Uislamu wa wazi na msafi kabisa usiokuwa na doa ni Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Na miongoni mwao kuna wakweli mno, mashahidi, waja wema na maimamu wenye kuongoza. Wana nafasi kuu na fadhilah zingine tulizozitaja. Miongoni mwao kuna wanaokuja kushika nafasi za wengine na maimamu wa dini ambao waislamu wameafikiana juu ya uwongofu wao. Nao ndio kundi lililonusuriwa ambalo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuwahusu:
“Hakutoacha kuwepo kikundi kutoka katika ummah wangu kuwa ni chenye kunusuriwa juu ya haki. Hatowadhuru wale wenye kwenda kinyume nao wala wenye kuwakosesha nusura mpaka kitapofika Qiyaamah.”[6]
Tunamuomba Allaah atujaalie katika wao, asizipotoshe nyoyo zetu baada ya kutuongoza na aturehemu – kwani hakika Yeye ndiye mwingi wa kutoa. Allaah ndiye mjuzi zaidi. Ee Allaah msifu na umsalimu Mtume wetu Muhammad, kizazi zake na Maswahabah wake wote.
MAELEZO
Wanaamini yale aliyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Mfano wa waumini katika kupendana kwao, kuhurumiana kwao na kuhisiana kwao ni kama mfano wa mwili mmoja. Wakati kiungo cha mwili kinapatwa na maumivu, basi mwili mzima unapatwa na homa na kukosa usingizi.”
Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Muumini kwa muumini mwenzake ni kama jengo; upande mmoja unaupa nguvu upande mwingine.”
“Muumini mwenye imani kamilifu zaidi ni yule mwenye tabia nzuri zaidi.”
Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni wenye kuyaamini yote haya. Katika yote wanayoyasema na kuyafanya ni wenye kufungamana na Qur-aan na Sunnah. Wao hawana malengo mengine. Bali maneno yao na matendo yao ni yenye kufungamana na Qur-aan na Sunnah. Kwa ajili hii ndio maana wakaitwa Ahl-us-Sunnah, watu wa Mkusanyiko na watu wa Qur-aan na Sunnah. Si kwa jengine bali ni kwa sababu wamekusanyika, kufungamana na kushirikiana katika hayo. Wao ndio Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah na watu wa Qur-aan na Sunnah. Hivi ndivyo walivyobainisha wanazuoni. Katika wao kuna maimamu wa uongofu na elimu. Hawa ni wale waliosimama barabara katika dini na wakajifungamanisha na Shari´ah. Wote hao wanaingia katika Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah.
Miongoni mwao kuna wale wanaokuja kushika nafasi za wengine. Hawa ni wale wenye kubadilishana baadhi kwa wengine. Hawa ni wale wanazuoni ambao baadhi wanawarithi wengine. Kwa maana ya kwamba anapokufa mwanachuoni huyu anakuja baada yake mwengine mpaka kifike Qiyaamah. Hii ndio hali ya ummah huu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakutoacha kuwepo kikundi kutoka katika ummah wangu kuwa ni chenye kunusuriwa juu ya haki. Hatowadhuru wale wenye kwenda kinyume nao wala wenye kuwakosesha nusura mpaka kitapofika Qiyaamah.”
Katika kipindi hicho waumini wanaume na wanawake wote watakuwa wameshafariki. Kutakuwa hakukubaki isipokuwa viumbe waovu tu ndio wataosimamiwa na Qiyaamah.
Tunamuomba Allaah atujaalie sisi na nyinyi kuwa katika wao, atukinge sisi na nyinyi kutokana na shari ya nafsi zetu na uovu wa matendo yetu na ainusuru dini Yake na alinyanyue Neno Lake. Hakuna nguvu za kufanya utiifu na kuacha maasi isipokuwa kwa msaada wa Allaah. Swalah na amani zimwendee mja na Mtume Wake na Mtume wetu Muhammad, jamaa zake na Maswahabah zake!
[1] al-Bukhaariy (2446) na Muslim (2585).
[2] al-Bukhaariy (6011) na Muslim (2586)
[3] Abu Daawuud (4682) na at-Tirmidhiy (1162). Nzuri na Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy.
[4] Abu Daawuud (4596), Ahmad (2/333), at-Tirmidhiy (2778). Ibn Maajah (3991) na wengine. Tazama “as-Silsilah as-Swahiyhah” (204) ya al-Albaaniy (Rahimahu Allaah).
[5] at-Tirmidhiy (2779) na al-Haakim (1/129).
[6] al-Bukhaariy (7311), Muslim (4951) na Ahmad (18135).
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 126
- Imechapishwa: 03/11/2024

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 126
Imechapishwa: 03/11/2024
https://firqatunnajia.com/82-hawa-ndio-ahl-us-sunnah-wal-jamaaah/