Baada ya hapo nuru hiyo imeongoza mioyo katika nuru kubwa na adhimu; nuru ya Sifa za Juu ambazo katika mng’ao wake nuru nyingine zote hufifia. Nuru hizo zikawa zinaishuhudia kwa macho ya imani na uhusiano wake kwa moyo ni kama ule wa vitu vinavyoonekana kwa jicho. Hayo ni kwa sababu ya kuenea kwa yakini juu yake na kufichuka kwa hakika za imani kwake, kiasi cha kuwa kana kwamba zinaona ´Arshi ya Mwingi wa rehema (Tabaarak wa Ta´ala) waziwazi na kulingana Kwake juu yake, kama alivyokhabarisha Mwenyewe (Subhaanahu wa Ta´ala) ndani ya Kitabu Chake na kama alivyokhabarisha Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Anaendesha mambo ya viumbe, anaamrisha na kukataza, anaumba na kuruzuku, anahuisha na kufisha, anahukumu na kutekeleza, anainua na kushusha, anabadilisha usiku na mchana, anafanya michana kupishana kati ya watu, anageuza dola kwa kuiondoa moja na kuleta nyengine. Wajumbe wa kimalaika wanapanda Kwake wakiwa na amri na hushuka kutoka Kwake nayo. Amri Zake na maamuzi Yake yanateremka kwa mpangilio kama wa Aayah, yanatekelezwa kwa mujibu wa matakwa Yake. Akitakacho hutokea kwa katika wakati anaoutaka na kwa namna atakayo, bila kuzidi, kupungua, kuchelewa wala kutangulia mbele. Amri Yake na ufalme Wake ni vyenye kuteketelezeka katika mbingu na pembezoni mwake, ardhini na vilivyomo na vilivyo chini yake, katika bahari na angani na katika kila sehemu ya ulimwengu na chembechembe zake. Anazigeuza, anazizungusha na anazifanya atakavyo. Amekizunguka kila kitu kiujuzi, amekidhibiti kila kitu kwa idadi, amekieneza kila kitu kwa huruma na hekima. Usikivu Wake unasikia sauti zote, pasi na kujali lugha na mahitaji. Hakumchanganyi wingi wa mambo kwa wakati mmoja. Hawachomshi wale wanaomuomba kwa masisitizo.
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 149-150
- Imechapishwa: 01/09/2025
Baada ya hapo nuru hiyo imeongoza mioyo katika nuru kubwa na adhimu; nuru ya Sifa za Juu ambazo katika mng’ao wake nuru nyingine zote hufifia. Nuru hizo zikawa zinaishuhudia kwa macho ya imani na uhusiano wake kwa moyo ni kama ule wa vitu vinavyoonekana kwa jicho. Hayo ni kwa sababu ya kuenea kwa yakini juu yake na kufichuka kwa hakika za imani kwake, kiasi cha kuwa kana kwamba zinaona ´Arshi ya Mwingi wa rehema (Tabaarak wa Ta´ala) waziwazi na kulingana Kwake juu yake, kama alivyokhabarisha Mwenyewe (Subhaanahu wa Ta´ala) ndani ya Kitabu Chake na kama alivyokhabarisha Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Anaendesha mambo ya viumbe, anaamrisha na kukataza, anaumba na kuruzuku, anahuisha na kufisha, anahukumu na kutekeleza, anainua na kushusha, anabadilisha usiku na mchana, anafanya michana kupishana kati ya watu, anageuza dola kwa kuiondoa moja na kuleta nyengine. Wajumbe wa kimalaika wanapanda Kwake wakiwa na amri na hushuka kutoka Kwake nayo. Amri Zake na maamuzi Yake yanateremka kwa mpangilio kama wa Aayah, yanatekelezwa kwa mujibu wa matakwa Yake. Akitakacho hutokea kwa katika wakati anaoutaka na kwa namna atakayo, bila kuzidi, kupungua, kuchelewa wala kutangulia mbele. Amri Yake na ufalme Wake ni vyenye kuteketelezeka katika mbingu na pembezoni mwake, ardhini na vilivyomo na vilivyo chini yake, katika bahari na angani na katika kila sehemu ya ulimwengu na chembechembe zake. Anazigeuza, anazizungusha na anazifanya atakavyo. Amekizunguka kila kitu kiujuzi, amekidhibiti kila kitu kwa idadi, amekieneza kila kitu kwa huruma na hekima. Usikivu Wake unasikia sauti zote, pasi na kujali lugha na mahitaji. Hakumchanganyi wingi wa mambo kwa wakati mmoja. Hawachomshi wale wanaomuomba kwa masisitizo.
Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 149-150
Imechapishwa: 01/09/2025
https://firqatunnajia.com/81-utawala-kamili-wa-muumba-juu-ya-viumbe/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket