80. Safari ya kupandishwa usiku ilikuwa katika hali ya macho

Miongoni mwa ´Aqiydah za maimamu wa Ahl-us-Sunnah, ni mamoja waliotangulia na waliokuja baadaye, ni pamoja na kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipandishwa katika mbingu ya juu kabisa, kwenye mkunazi wa mpaka wa mwisho kabisa, ambapo akawa kiasi cha umbali wa mipinde miwili au karibu zaidi.

Hapo ndipo Allaah alipomfaradhishia swalah tano. Wakati wa tukio hilo alimpitia Muusa (´alayhis-Salaam), akamweleza kuwa yeye aliwajaribu watu jambo hilo kabla yake na kwamba watu wake hawatoweza, ambapo akamuomba arejee kwa Mola wake na amwombe ampunguzie. Baadhi ya Hadiyth zinazozungumzia safari ya kupandishwa mbinguni zimekwishatangulia. Ni ndefu na zenye kutambulika. Haafidhw ´Abdul-Ghaniy amezikusanya katika mijeledi miwili. Ingelikuwa kupandishwa kwake mbinguni (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni kwa njia ya usingizi na kwamba kushuka kwake katika kupanda kwake katika mkunazi wa mpaka wa mwisho ni ndoto na jambo la kufikiria peke yake, kama wanavyoona baadhi ya watambuzi, basi kusingelikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na sifa yoyote kubwa ya kipekee kuliko waja wema wengi wa ummah wake. Na wala wa Haki (´Azza wa Jall) asingethibitisha kupandishwa kwake mbinguni na akathibitisha ilikuwa katika hali ya kuwa macho na yenye kuonekana kwa macho. Kwa sababu amesema (´Azza wa Jall):

إِذْ يَغْشَى السِّدْرَةَ مَا يَغْشَىٰ مَا زَاغَ الْبَصَرُ وَمَا طَغَىٰ

”… pindi ulipoufunika mkunazi huo unachokifunika, jicho lake halikukengeuka wala halikupinduka mipaka.”[1]

Mwanachuoni wa ummah huu Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) amesema:

”Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliona jambo hilo kwa macho yake.”

[1] 53:16-17

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk. 116
  • Imechapishwa: 01/07/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy