2- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza:

“Hakika Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ´Alikuwa akiliswalia jeneza husema:

اللهم اغفر لحينا وميتنا، وشاهدنا وغائبنا، وصغيرنا وكبيرنا، وذكرنا وأنثانا، اللهم من أحييته منا فأحيه على الاسلام، ومن توفيته منا فتوفه على الايمان، اللهم لا تحرمنا أجره، ولا تضلنا بعده

“Ee Allaah! Msamehe aliyehai katika sisi na aliyekufa katika sisi, aliyepo na asiyekuwepo, wadogo wetu na wakubwa wetu, wakiume wetu na wakike wetu.  Ee Allaah! Ambaye utampa uhai katika sisi basi mpe uhai katika Uislamu na utayemfisha katika sisi basi mfishe juu ya imani.  Ee Allaah! Usitunyime ujira Wake na wala usitupoteze baada ya yeye kuondoka.”

Ameipokea Ibn Maajah (01/456), al-Bayhaqiy (04/41) kupitia njia ya Muhammad bin Ibraahiym at-Taymiy kutoka kwa Abu Salamah kutoka kwake.

Abu Daawuud (02/68), at-Tirmidhiy (02/141), Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” yake (757- Mawaarid), al-Haakim (01/358), al-Bayhaqiy pia na Ahmad (02/368) kupitia kwa njia ya Yahyaa bin Abiy  Kathiyr kutoka kwa Abu Salamah ambaye amepokea mfano wake pasi na “Ee Allaah! Usitunyime… “ Iko kwa Abu Daawuud peke yake. Yahyaa amesema kwa wazi kwamba amehadithia kwa al-Haakim kisha akasema:

“Ni Swahiyh juu ya sharti za al-Bukhaariy na Muslim”. adh-Dhahabiy akaafikiana naye, mambo ni kama walivosema. Imetiwa dosari kwa kitu kisichotiwa dosari.

Yahyaa anazo cheni mbili za wapokezi wengine kwa Ahmad (04/170-308) na al-Bayhaqiy.

Hadiyth inayo shahidi kutoka katika Hadiyth ya Ibn ´Abbaas mfano wake.

Ameipokea at-Twabaraaniy katika “al-Kabiyr”.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 157-158
  • Imechapishwa: 06/02/2022