Ili mtu aweze kumwangalia mwanamke ambaye anataka kumchumbia inatakiwa isiwe faragha. Dalili ya hilo ni jumla ya Hadiyth ambazo zinakataza mwanaume kuwa faragha na mwanamke ajinabi. Haifai kumwangalia ikiwa hayuko na Mahram wake. Hakuna dalili maalum juu ya hilo. Hapa kutabainika makosa yanayofanywa na watu sampuli mbili:
1- Wakati mchumba anapokuja kwa mlezi na kumkinaisha kuwa anataka kumchumbia mwanamke na hivyo akataka kumuona, mlezi anasema kuwa hawana wasichana wenye kuangaliwa.
2- Wakati mchumba anapokuja kwa mlezi na kumuomba hali kadhalika, mlezi anamwambia amchukue na aende kutembea naye, aende kula naye, kaa naye, zungumza naye, pataneni, juaneni, zisomeni tabia zenu na kila kitu. Sivyo tu, bali anamwacha akae naye faragha kwenye chumba ili waweze kuzungumza.
Hali zote hizi mbili ni zenye kulaumika. Hali ya kati na kati ni ile aliyoelekeza Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mwanaume amwangalie mwanamke pasina kuwa faragha. Amwangalie wakati yuko na mlezi wake.
- Muhusika: Shaykh Sulaymaan bin Saliym ar-Ruhayliy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Haqq-uz-Zawjayn, uk. 15-16
- Imechapishwa: 24/03/2017
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)
Related
Mahusiano kati ya mchumba na mchumbiwaji
Swali: Ni upi mpaka wa mahusiano kati ya yule mchumba (خاطب) na mchumbiwaji (مخطوبة)? Je, inafaa kwake kuwa naye faragha na kwenda nae? Jibu: Hapana, haijuzu. Isipokuwa ikiwa kama atafunga naye ndoa. Hatakiwi kuwa naye faragha. Akitaka kutazama yale yatayomvutia kwa ajili ya kumposa; basi hayo yanatakiwa kufanywa mbele ya…
In "Uchaguzi wa mke na mume"
Dereva kuwa faragha na msichana
Swali: Miongoni mwa sababu za kuenea kwa uzinzi ni madereva na wafanyakazi kuwa wengi. Hayo yanaonekana vyuoni, katika masomo ya wasichana, masoko na minasaba mbalimbali. Ni yepi maelekezo yako? Je, inafaa kumwingiza nyumbani mfanyakazi msichana mdogo kwenye nyumba ambayo imejaa wavulana au kuwepo dereva pamoja na wasichana wenye umri mdogo.…
In "Mwanamke na safari"
Mama na wasichana zake kwenda sokoni na dereva wa kiume
Swali: Mimi ni baba na nina watoo ambapo tunakuwa tumeshughulishwa na kazi zetu. Kwa ajili hiyo tunamruhusu dereva aende sokoni, mihadhara ya kidini na ya kiutamaduni pamoja na mke na wasichana wangu. Naomba jawabu la kutosha juu ya kitendo hichi juu ya uhalali au uharamu wake. Jibu: Ni sawa endapo dereva…
In "Mwanamke na safari"