81- Aombe ndani yake zile du´aa zilizothibiti kutoka kwake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Katika hizo nimesimamia nne:
1- ´Awf bin Maalik (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia: “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimswalia maiti ambapo nikahifadhi kutoka katika du´aa yake akisema:
اللهم اغفر له وارحمه، وعافه واعف عنه، وأكرم نزله، ووسع مدخله، واغسله بالماء والثلج والبرد، ونقه من الخطايا كما نقيت (وفي رواية: كما ينقي) الثوب الابيض من الدنس، وأبدله دارا خيرا من داره، وأهلا خيرا من أهله، وزوجا (وفي رواية: زوجة) خيرا من زوجه، وأدخله الجنة، وأعذه من عذاب القبر، ومن عذاب النار، قال: فتمنيت أن أكون أنا ذلك الميت
“Eee Allaah! Mghufurie na mrehemu, muafu na msamehe na mtukuze kushuka kwake [kaburini] na mpanulie maingilio yake na muoshe na maji na kwa theluji na barafu na mtakase na makosa kama Ulivyoitakasa nguo (katika upokezi mwingine imekuja: “Kama inavotakaswa) nguo nyeupe kutokamana na uchafu na mbadilishie nyumba bora kuliko nyumba yake na jamaa bora kuliko jamaa zake na mume (katika upokezi mwingine imekuja: mke) bora kuliko mke wake na mwingize Pepo na mlinde na adhabu ya kaburi na adhabu ya Moto.”
Msimuliaji amesema: “Nilitamani mimi ndiye niwe huyo maiti.”
Ameipokea Muslim (03/59-60), an-Nasaa´iy (01/271), Ibn Maajah (01/4256), Ibn-ul-Jaaruud (264-265), al-Bayhaqiy (04/40), at-Twayaalisiy (999), Ahmad (06/23, 28) na mtiririko ni wa Muslim, upokezi wa pili ni wake katika moja ya upokezi, na ni wa waliosalia isipokuwa Ahmad na al-Bayhaqiy anao upokezi wa tatu.
Katika upokezi wa Ibn Maajah na at-Twayaalisiy imetajwa kwamba maiti alikuwa ni mwanamme wa ki-Answaar. Lakini katika cheni ya wapokezi wake yuko Faraja bin Fadhwaalah – naye ni mnyonge – kutoka kwa ´Iswmah bin Raashid ambaye hatambuliki.
Hadiyth ameitoa at-Tirmidhiy (02/141) mukhtasari ambaye amesema:
“Hadiyth ni geni na Swahiyh. Muhammad bin Ismaa´iyl amesema – yaani al-Bukhaariy –Hadiyth ambayo ni Swahiyh zaidi kuhusiana na maudhui haya ni hii.”
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 157
- Imechapishwa: 06/02/2022
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
39. Sifa ya kumswalia maiti
Swali 39: Tunatumai utuwekee wazi namna ya kuswalia jeneza kama ilivyothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Kwani watu wengi hawajui[1]. Jibu: Sifa ya kuswalia jeneza ni jambo amelibainisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake (Radhiya Allaahu ´anhum). Mosi anatakiwa kusema “Allaahu Akbar”, aombe kinge…
In "Ahkaam-ul-Janaa-iz - Ibn Baaz"
44. Namna ya kukamilisha swalah ya jeneza kwa aliyejiunga amechelewa
Swali 44: Mswaliji anatakiwa kulipa swalah ya jeneza akiingia akakuta amekwishapitwa na baadhi ya sehemu yake[1]? Jibu: Atailipa papo hapo. Akijiunga na imamu katika Takbiyr ya tatu basi ataleta Takbiyr na kusoma al-Faatihah. Pindi imamu atapoleta Takbiyr ya nne basi naye ataleta Takbiyr ya pili kwa nisba yake na atamswalia…
In "Ahkaam-ul-Janaa-iz - Ibn Baaz"
80. Du´aa ya pili ya kumuombea maiti
2- Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza: “Hakika Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ´Alikuwa akiliswalia jeneza husema: اللهم اغفر لحينا وميتنا، وشاهدنا وغائبنا، وصغيرنا وكبيرنا، وذكرنا وأنثانا، اللهم من أحييته منا فأحيه على الاسلام، ومن توفيته منا فتوفه على الايمان، اللهم لا تحرمنا أجره، ولا تضلنا بعده…
In "13. Mlango wa kumi na tatu: Mlango wa kumi na tatu: Kuhusu kumswalia mtoto na aliyekufa shahidi"