77. Ndio maana wanazuoni wakaweka mlango wa mwenye kuritadi

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Yaweza kusemwa pia: “Ikiwa [watu] wa mwanzo hawakukufuru, isipokuwa kwa kujumuisha kwao baina ya shirki, kumkadhibisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Qur-aan na kupinga kufufuliwa na kadhalika, ni nini maana ya mlango uliotajwa na wanachuoni wa kila madhehebu “Mlango unaozungumzia hukumu ya mwenye kuritadi”, naye ni yule muislamu ambaye anakufuru baada ya kuwa muislamu? Halafu wakataja aina nyingi; kila aina inakufurisha na kuhalalisha kumwagwa damu ya mtu na mali yake. Mpaka wakataja mambo ambayo yalionekana ni madogo kwa yule mwenye kuyafanya, kama mfano maneno yaliosemwa na mdomo wake bila ya kuyamaanisha [kuyakusudia] moyoni mwake au maneno aliyosema kwa njia ya mzaha na utani.

MAELEZO

Hili ni jibu la sita. Ikiwa washirikina waliotangulia hawakukufuru isipokuwa baada ya kukusanya aina zote za kufuru kama shirki, ukadhibishaji na kiburi, ni ipi basi maana ya zile aina mbalimbali za kufuru zilizotajwa katika mlango wa hukumu ya mwenye kuritadi? Kila aina inasababisha kukufuru. Walifikia mpaka kutaja mambo yaliyokuwa yakionekana hayana maana kwa wale wenye kuyafanya. Kwa mfano ni neno analolitamka mtu mdomoni pasi na kulimaanisha moyoni au mzaha na mchezo. Ikiwa mambo haya hayasababishi kufuru, basi kusingekuwa na faida yoyote kuyataja, hata kama wenye kuyafanya wanaweza kuwa wazuri kwa mtazamo mwingine.

Anasema (Rahimahu Allaah) ya kwamba wanazuoni wa Fiqh wa kila madhehebu wameraddi utata wa watu hawa wanapofika katika mlango wa hukumu ya mwenye kuritadi. Humo wametaja aina nyingi za kufuru. Wamefikia mpaka kutaja mambo ambayo yalikuwa yanaonekana hayana maana kwa wale wenye kuyatenda. Mfano wa hilo ni neno analolitamka mtu pasi na kumaanisha hivo moyoni au kwa mzaha. Pamoja na hivyo walimkufurisha na wakawatoa katika Uislamu kwa sababu ya matendo haya. Suala hili litatajwa kwa ubainifu na uwazi zaidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 86-87
  • Imechapishwa: 25/11/2023