Swali 77: Magazeti ya leo yanaandika kususia bidhaa za kimarekani kwa njia ya kutozinunua wala kuziuza. Wanasema kuwa wanazuoni wanahimiza zisuswe na kwamba kitendo hichi ni cha lazima kwa waislamu wote na kwamba mwenye kufanya hivo ni haramu na kwamba ametenda dhambi kubwa na kwamba amewasaidia watu watu hao na mayahudi dhidi ya kuwapiga vita waislamu. Unaweza kuweka wazi jambo hilo? Je, mtu analipwa thawabu kwa kitendo hicho?

Jibu: Hilo si sahihi. Wanazuoni hawakutoa fatwa juu ya uharamu wa kufanya biashara za kimarekani. Bidhaa za kimarekani bado ziko katika masoko ya waislamu.

Bidhaa hazigomewi isipokuwa pale ambapo mtawala atazipiga marufuku na akaamrisha kuisusa nchi fulani. Katika hali hiyo ndio italazimika kuzisusa. Ama wananchi hawana haki ya kutoa fatwa ya kuharamisha. Kwa sababu fatwa kama hizo maana yake ni kuharamisha vile alivyohalalisha Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 194-195
  • Imechapishwa: 17/07/2024