76. Miaka mia saba baina ya sikio na mabega

75 – Jaabir amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Nimepewa ruhusa ya kumsimulia mmoja katika wale Malaika wanaobeba ´Arshi. Umbali kutoka sehemu ya sikio hadi mabega yake ni masafa ya miaka mia saba.”

Cheni yake ya wapokezi ni Swahiyh[1].

[1] Mambo ni kama alivosema. Ameipokea Abu Daawuud na wengineo. Nimeikagua katika ”as-Swahiyhah” (151).

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk. 114-115
  • Imechapishwa: 30/06/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy