Kundi la kwanza ni warithi wa Mitume na wale wanaokuja kuchukua sehemu za Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam). Nao ni wale walionyooka barabara juu ya dini kwa elimu, matendo na ulinganizi kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall) na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hawa ndio wafuasi wa kweli wa Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam). Wao ni sawa na sehemu nzuri ya ardhi ambayo imetakata, ikapokea maji, kisha ikachipuza majani na nyasi nyingi. Basi ikatakata yenyewe na watu wakatakata kwao. Hawa ndio waliochanganya baina ya utambuzi katika dini na nguvu ya kuilingania na kwa ajili hiyo wakawa ndio warithi wa Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) ambao Allaah (Ta´ala) amesema kuhusu wao:
وَاذْكُرْ عِبَادَنَا إِبْرَاهِيمَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ أُولِي الْأَيْدِي وَالْأَبْصَارِ
“Wakumbuke waja Wetu – Ibraahiym na Ishaaq na Ya’quub – wenye nguvu na busara.”[1]
Kwa utambuzi na ufahamu juu ya dini ya Allaah (´Azza wa Jall). Kwa utambuzi na ufahamu wanaweza kuielewa na kuitambua haki, kwa nguvu wanaweza kuifikisha kwa wengine na kutekelezwa pamoja na kulingania kwayo. Kundi hili lina nguvu inapokuja katika hifdhi, ufahamu wa dini na uelewa wa tafsiri. Wanachimbua kutoka katika Maandiko mito ya elimu, ikatoa humo hazina zake na wakaruzukiwa humo uelewa maalum. Kama alivosema Kiongozi wa waumini ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) alipoulizwa kama Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwahusisha na kitu maalum kisichokuwa kwa watu wengine:
“Hapana, naapa kwa Yule aliyepasua punje na kuumba nafsi! Isipokuwa tu uelewa ambao Allaah humpa mja katika Kitabu Chake.”[2]
Huu uelewa ni kama majani na nyasi nyingi zilizochipuka kutoka ardhini.
[1]38:45
[2] al-Bukhaariy (3047).
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 135-136
- Imechapishwa: 26/08/2025
Kundi la kwanza ni warithi wa Mitume na wale wanaokuja kuchukua sehemu za Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam). Nao ni wale walionyooka barabara juu ya dini kwa elimu, matendo na ulinganizi kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall) na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Hawa ndio wafuasi wa kweli wa Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam). Wao ni sawa na sehemu nzuri ya ardhi ambayo imetakata, ikapokea maji, kisha ikachipuza majani na nyasi nyingi. Basi ikatakata yenyewe na watu wakatakata kwao. Hawa ndio waliochanganya baina ya utambuzi katika dini na nguvu ya kuilingania na kwa ajili hiyo wakawa ndio warithi wa Mitume (Swalla Allaahu ´alayhim wa sallam) ambao Allaah (Ta´ala) amesema kuhusu wao:
وَاذْكُرْ عِبَادَنَا إِبْرَاهِيمَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ أُولِي الْأَيْدِي وَالْأَبْصَارِ
“Wakumbuke waja Wetu – Ibraahiym na Ishaaq na Ya’quub – wenye nguvu na busara.”[1]
Kwa utambuzi na ufahamu juu ya dini ya Allaah (´Azza wa Jall). Kwa utambuzi na ufahamu wanaweza kuielewa na kuitambua haki, kwa nguvu wanaweza kuifikisha kwa wengine na kutekelezwa pamoja na kulingania kwayo. Kundi hili lina nguvu inapokuja katika hifdhi, ufahamu wa dini na uelewa wa tafsiri. Wanachimbua kutoka katika Maandiko mito ya elimu, ikatoa humo hazina zake na wakaruzukiwa humo uelewa maalum. Kama alivosema Kiongozi wa waumini ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh) alipoulizwa kama Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliwahusisha na kitu maalum kisichokuwa kwa watu wengine:
“Hapana, naapa kwa Yule aliyepasua punje na kuumba nafsi! Isipokuwa tu uelewa ambao Allaah humpa mja katika Kitabu Chake.”[2]
Huu uelewa ni kama majani na nyasi nyingi zilizochipuka kutoka ardhini.
[1]38:45
[2] al-Bukhaariy (3047).
Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 135-136
Imechapishwa: 26/08/2025
https://firqatunnajia.com/75-udongo-wa-ummah-uliyo-na-rutuba/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket