75. Tofauti kati ya kuwa juu kwa Allaah na kulingana Kwake

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

Mara sita Amesema:

ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ

“… kisha akalingana juu ya ´Arshi.”[1]

الرَّحْمَـٰنُ عَلَى الْعَرْشِ اسْتَوَىٰ

”Mwingi wa rehema amelingana juu ya ´Arshi.”[2]

MAELEZO

Maeneo sita ndani ya Qur-aan imekuja:

ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ

“… kisha akalingana juu ya ´Arshi.”

Bi maana amepanda na kuwa juu yake. Kulingana ni moja miongoni mwa sifa za Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) za kimatendo, ilihali ujuu ni sifa ya kidhati. Tofauti kati ya ujuu wa Allaah na kulingana Kwake juu ni kwamba Allaah daima anasifika kuwa juu ilihali kulingana ni sifa ya kimatendo anayoifanya pale anapotaka. Ndio maana akasema:

ثُمَّ اسْتَوَىٰ عَلَى الْعَرْشِ

“… kisha akalingana juu ya ´Arshi.”

Kielezi ”kisha” kinaonyesha mpangilio wa matukio. Kwa hivyo kulingana ni sifa ya kimatendo Anayoifanya wakati anapotaka (Subhaanahu wa Ta´ala), ilihali ujuu Wake ni sifa ya kidhati ambayo daima anasifika nayo. Katika Suurah ”al-A´raaf”, ”Yuunus”, ”ar-Ra´d”, ”Twaa Haa”, ”al-Furqaan”, ”as-Sajdah” na ”al-Hadiyd” Allaah amethibitisha kulingana juu ya ´Arshi.

[1] 07:54

[2] 20:05

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat at-Tawdhwiyhiyyah ´alaa Muqaddimat-il-Fatwaaa al-Hamawiyyah, uk. 112-113
  • Imechapishwa: 20/08/2024