Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
127 – Uko kati ya kuchupa mipaka na kuzembea, kufananisha na kukanusha, utenzwaji nguvu na makadirio, usalama na kukata tamaa.
128 – Hii ndio dini na ´Aqiydah yetu, kwa nje na kwa ndani.
129 – Sisi tunajitenga mbali kutokana na ambaye anaenda kinyume na yale yote tuliyoyataja na kuyabainisha.
130 – Tunamuomba Allaah (Ta´ala) atuthibitishe juu ya imani na atufishe katika hali hiyo.
131 – Tunamuomba atukinge kutokana na matamanio yanayotofautiana, fikira zinazotofautiana na madhehebu mabaya kama mfano wa Mushabbihah, Mu´tazilah, Jahmiyyah, Jabriyyah, Qadariyyah na wengine wote ambao wanaenda kinyume na Sunnah na mkusanyiko na wakakumbatia upotofu. Sisi tunajitenga mbali na wao na tunawazingatia kuwa ni wapotofu na wabaya[1] – Allaah ndiye Mwenye kulinda na kuwafikisha.
MAELEZO
Miongoni mwao ni wale wenye kufuata kichwa mchunga ambao wamefanya kufuata kibubusa ni dini ya wajibu ambayo analazimika kuifuata kila ambaye amekuja baada ya karne ya nne. Matokeo yake wakavipa mgongo kufuata mwongozo wa Qur-aan na Sunnah na pia wakamtuhumu kila yule ambaye amejaribu kujinasua na ufuataji wa kipofu wa madhehebu na kushikamana na uongofu wake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah amrehemu imamu wa Sunnah, ambaye amesema:
Dini ya Muhammad ni maelezo
uzuri uliyoje wa mapokezi kwa kijana!
Usizipe mgongo Hadiyth na watu wake
kwa sababu maoni ni usiku na Hadiyth ni mchana
[1] Baada ya haya imekuja katika moja ya nakala:
”Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ndiye mwenye kuongoza katika haki. Haya ndio yote tuliyokusudia na kuyaashiria. Himdi zote anastahiki Allaah, Mola wa walimwengu.”
Swalah na amani zimwendee bwana wetu Muhammad, kizazi chake na Maswahabah zake.
Dameski, jumamosi 19 Jumaadaa al-Uulaa 1394.
Usafishaji wa uandishi umemalizika siku ya jumatatu 5 Jumaadaa al-Aakhirah 1394 na umefanywa na ´Abdul-Musawwir bin Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy. Siku ya kufuatia nilikihakikisha kitabu kwa ambacho ni cha asili. Swalah na amani zimwendee Muhammad, kizazi chake na Maswahabah zake wote. Himdi zote ni stahiki ya Allaah, Mola wa walimwengu.
Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 110-112
- Imechapishwa: 27/10/2024

Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 110-112
Imechapishwa: 27/10/2024
https://firqatunnajia.com/75-sunnah-ni-jua/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket