75. Mtu kumzungumzia mwengine msiba wake kunaiathiri subira

Miongoni mwa mambo yanayoathiri subira na ridhaa ya mwenye kupatwa na msiba ni kuuonyesha msiba ule na kuwaeleza nao wengine. Haijalishi kitu sawa ikiwa atawaeleza marafiki zake au wengine. Isipokuwa tu ikiwa kama atasema kuwaambia jamaa au marafiki zake ya kwamba baba au mtoto wa fulani amefariki na akawa hakukusudia kuuonyesha msiba wake. Katika hali hiyo makusudio yake iwe amewajuza ili wamuombee, washindikize jeneza lake na mambo mengine ambayo ni faradhi kwa baadhi ya waislamu. Kwa njia hiyo watapata thawabu zilizo sawa na mlima.

Wakati ´Atwaa´ alipokuwa kipofu kwenye jicho moja ilichukua miaka ishirini kabla hata ya familia yake kujua hilo. Ilikuja kutambulika pindi mtoto wake alipokuja upande ule wa jicho lake lisiloona bila ya yeye kujua hilo ndipo wakajua kuwa Shaykh jicho lake limoja limepofoka.

Kuna mwanaume alikuja kwa Daawuud at-Twaa-iy akamuona anatambaa chini. Alioyaona yakamfanya aseme: “Hakika sisi ni wa Allaah na hakika sisi Kwake ni wenye kurejea.” Daawuud akasema: “Kimya! Usimwambie yeyote.” Kabla ya hapo alikuwa akisaidiwa kukaa kwa miezi minne pasi na mtu yeyote kujua hilo.”

al-Ahnaaf alimshtakia mara kwa mara baba yake juu ya maumivu ya jino. Ndipo baba yake akamwambia:

“Acha kulalamika. Nilipoteza jicho langu kwa miaka arubaini iliyopita na sikumlalamikia yeyote.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Muhammad al-Hanbaliy al-Manbajiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Tasliyatu Ahl-il-Maswaa-ib, uk. 167
  • Imechapishwa: 13/11/2016