75. Hivi ndivo alivyouliwa dogo al-Haarith bin Suraaqah

74 – Anas amesimulia kwamba baada ya mtoto wa kiume al-Haarith bin Suraaqah wa ar-Rubayy´ bint an-Nadhwr kuuliwa siku ya Badr, alimjia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kusema:

”Ee Mtume wa Allaah, nipe khabari kuhusu Haarithah? Akiwa yuko Peponi, basi nitataraji malipo na kusubiri. Na ikiwa hakuingia Peponi, basi nitajitahidi katika kuomba du´aa.” Akasema: ”Ee Umm Haarithah! Kuna mabustani Peponi. Mtoto wako amepata Firdaws ya juu kabisa. Firdaws ni kilima cha Pepo, ya katikati yake na bora yake. Bi maana juu yake kuna ´Arshi ya Mwingi wa rehema (´Azza wa Jall).”[1]

Imekuja katika njia nyingine:

”Haarithah alikuwa tu ni kijana na alitoka kwenda Badr kuangalia na sio kwa ajili ya kupigana. Ukampata mshale kifuani mwake na kumuua.”

[1] Mpaka hivi sasa sijapata tamko lisemalo ”juu yake kuna ´Arshi ya Mwingi wa rehema (´Azza wa Jall)”. Mtunzi ameipokea katika ile ya asili kupitia kwa Rawh bin ´Ubaadah: Ibn Abiy ´Aruubah ametuhadithia, kutoka kwa Qataadah, kutoka kwa Anas.   Hakuiegemeza kwa mtunzi yeyote, kama ilivyo kawaida yake mara nyingi. at-Tirmidhiy ameipokea kwa njia hiyohiyo kwenda mpaka ”Firdaws ni kilima cha Pepo, ya katikati yake na bora yake” pasi na ziada na akasema ”Hadiyth ni nzuri na Swahiyh”. Vivyo hivyo amefanya Ahmad (3/260) kupitia kwa Shaybaan, kutoka kwa Qataadah. Hata hivyo amefanya sentesi ya mwisho ni yenye kujuimuishwa katika Hadiyth. Amesema: ”Qataadah amesema ´Firdaws ni kilima cha Pepo, ya katikati yake na bora yake`.” al-Bukhaariy ameipokea (02/204) kupitia njia hiyohiyo, hata hivyo pasi na ziada iliyojumuishwa wala kwamba ni maneno ya Qataadah. Abaan amefuatilia upokezi huo na akasimulia yale ambayo Qataadah amewaeleza, ameyapokea Ahmad (03/283). Humayd amemfuatilia na akasimulia kwamba amemsikia Anas akiisimulia, ameipokea Ahmad na al-Bukhaariy (3/59) na (4/241). Thaabit al-Bunaaniy ameifuatilia kutoka kwa Anas kwa ile jumla ya mwisho iliyotajwa, ameipokea Ahmad (3/124, 215, 272 na 282). Cheni zote hizi za wapokezi hazina hiyo ziada iliyojumuishwa wala ile ziada ya kwanza. Nakhofia kwamba mtunzi (Rahimahu Allaah) ameteleza. Lakini ziada hiyo iko katika Hadiyth (14) ya Abu Hurayrah iliyotangulia. Imekaguliwa katika ”as-Swahiyhah” (918). Muda ulivyokuwa unaenda ziada hiyo ikanibainikia kuwa ni yenye kutoka kwa mtunzi kwa njia ya kubainisha na kupambanua. Uchapishaji ulidondosha jumla inayosema ”bi maana”na hivyo utata umeondoka. Utata huo umeondoka baada ya mimi kurekebisha katika muswada.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk. 113-114
  • Imechapishwa: 30/06/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy