74. Wanandugu kwa ajili ya Allaah

Moja katika njia mbili zilizoashiriwa imepokelewa na Abu Idriys, kutoka kwa Mu´aadh. Mtunzi ameitaja katika ile ya asili ambapo akaikosoa kukatika na kusema:

”Sahihi ni kwamba Abu Idriys hakuwahi kuzungumza na Mu´aadh bin Jabal ingawa waliishi wakati mmoja.”

Hivo ndivo alivosema (Rahimahu Allaah), maoni aliyochukua kutoka kwa Abu Zur´ah na wanazuoni wengine waliotangulia. Hata hivyo Haafidhw Ibn ´Abdil-Barr kathibitisha kusikia kutoka kwake. Maoni haya ndio yenye nguvu zaidi, khaswa kwa kuzingatia kwamba Hadiyth hii aliisikia kutoka kwake. Hilo limethibiti kupitia njia mbili kutoka kwake:

1 – Kutoka kwa Shu´bah, kutoka kwa Ya´laa bin ´Atwaa’, kutoka kwa al-Waliyd bin ´Abdir-Rahmaan, kutoka kwa Abu Idriys al-Khawlaaniy, aliyesema:

”Niliikaa kwenye kikao ambacho kilikuwa na Maswahabah ishirini wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kati yao alikuwepo kijana mmoja mzuri… Alikuwa ni Mu´aadh bin Jabal (Radhiya Allaahu ´anh). Siku iliyofuata nikaja na kumkuta akiswali kwenye nguzo. Akaswali swalah fupi, akaketi chini na magoti yake na kunyamaza.” Nikamwambia: ”Mimi nakupenda kutokana na utukufu wa Allaah.” Akasema: ”Unaapa kwa Allaah?” Nikasema: ”Naapa kwa Allaah.”

Kisha akataja masimulizi hayo kutoka kwa Mu´aadh. Ameipokea Ahmad na al-Haakim.

2 – ´Atwaa´ al-Khuraasaaniy amesema: ”Nimemsikia Abu Idriys al-Khawlaaniy akisema:

”Niliingia katika msikiti wa Himsw na nikaketi chini kwenye duara ya kielimu ambapo wote walikuwa wakisimulia kutoka kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kati yao alikuweko kijana mzuri… ”

Akataja Hadiyth mfano wake. Ameipokea al-Haakim.

3 – Maalik amepokea katika ”al-Muwattwa´” (02/953/16) Hadiyth ya tatu na kupitia kwake Ibn Hibbaan, kutoka kwa Abu Haazim bin Diynaar, kutoka kwa Abu Idriys al-Khawlaaniy, ambaye amesema:

”Niliingia msikitini huko Dameski na nikamuona kijana mwenye meno ya mbele yanayong’aa. Alikuwa na watu. Pale wanapotofautiana juu ya jambo, basi wanalirejesha kwake ambapo wakayafanyia kazi maneno yake. Nikauliza ni nani na nikaambiwa kuwa ni Mu´aadh bin Jabal. Siku inayofuata nikaondoka mapema na nikakuta ameshanitangulia. Nikamkuta akiswali. Nikasubiri amalize kuswali kisha nikamwendea, nikasimama mbele ya uso wake, nikamsalimia na kusema: ”Naapa kwa Allaah kwamba mimi nakupenda kwa ajili ya Allaah.”

Akataja Hadiyth kama hiyo yenye tofauti:

”Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema: ”Yamethibiti mapenzi Yangu juu ya wale wanaopendana kwa ajili Yangu, wanaokaa kwa ajili Yangu, wanaotembeleana kwa ajili Yangu na wanaofanyiana huduma kwa ajili Yangu.”

Kuafikiana wasimulizi wote hawa watatu ambao ni madhubuti kunathibitisha kusikia kwa Abu Idriys kutoka kwa Mu´aadh bin Jabal, jambo ambalo ni vigumu sana kulipuuza na kuona kuwa ni udanganyifu – na Allaah ndiye mjuzi zaidi.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk. 113
  • Imechapishwa: 26/06/2024
  • taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy