Mifano hii miwili inafanana na mifano miwili mingine iliyotajwa katika Suurah ”ar-Ra´d” pale aliposema (Ta´ala):
أَنزَلَ مِنَ السَّمَاءِ مَاءً فَسَالَتْ أَوْدِيَةٌ بِقَدَرِهَا فَاحْتَمَلَ السَّيْلُ زَبَدًا رَّابِيًا
”Ameteremsha kutoka mbinguni maji na mabonde yakatiririka kwa kiwango chake, halafu mbubujiko ukabeba mapovu ya takataka yanayopanda juu yake.”[1]
Huu ndio mfano wa maji. Amefananisha (Ta´ala) na wahy, ambao umeteremshwa ili kuzihuisha nyoyo, kama ambavyo maji aliyoteremsha kutoka mbinguni yanayoihuisha ardhi. Amezifananisha nyoyo zinazoibeba hiyo elimu na uongofu na mito inayobeba maji. Basi moyo mkubwa una uwezo wa kubeba elimu kubwa kama vile mto mkubwa unavyoweza kubeba maji mengi. Moyo mdogo ni kama mto mdogo unaobeba kiasi kidogo cha elimu. Nyoyo zimechukua kutoka katika elimu hiyo kwa kiwango chao kama vile mito ilivyofurika kwa kiwango chake.
Wakati ilipokuwa mito na njia za mito ndani yake kuna takataka na vinginevyo vinavyochukuliwa na mto na kubebwa juu ya maji, povu lililoinuka juu yake huenea juu kwa wingi. Lakini chini yake kuna maji matamu ambayo ndio yanayoihuisha ardhi. Kisha mto hutupa povu hilo pembeni mwa mto mpaka kubaki maji safi chini ya povu, kisha Allaah anamnywesha nayo ardhi na hivyo anaihuisha nchi, watu, miti na wanyama. Povu linaenda bure na linatupwa pembeni mwa mto.
Vivyo hivyo elimu na imani aliyoiteremsha ndani ya nyoyo ambapo nyoyo zikabeba hiyo elimu na ikatokeza humo kutokana na kuchanganyika kwake na hiyo elimu kile kilichoko ndani yao cha takataka za matamanio na povu la shubuha batili likajitokeza juu yao. Elimu, imani na uongofu vinabakia katika mizizi ya moyo. Povu hilo na takataka huondoka kidogo kidogo mpaka yote yameondoka na kubakia elimu yenye manufaa na imani safi ndani ya mizizi ya moyo. Basi watu huifikia ambapo kunywa, kunywesha na kupata malisho. Kama alivyosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Mfano wa yale niliyotumilizwa na Allaah katika uongofu na haki ni kama mfano wa mvua nyingi iliyonyesha katika ardhi ambapo ikawa nzuri, ikakubali maji na kuotesha nyasi na majani mengi. Sehemu nyingine ikawa ni kavu na ngumu inayozuia maji, Allaah akawanufaisha watu kwa mvua hiyo ambapo wakanywa [mifugo yao] na wakalima [kwa maji hayo]. Ikanyesha sehemu nyingine ambayo ni kame haizuii maji na wala haioteshi nyasi. Basi mifano hiyo ni mfano wa mtu aliyefahamu katika dini ya Allaah, Allaah akamnufaisha na yale aliyonituma kwayo, akajua na akafundisha [wengine]. Na mfano [wa aina hii ya mwisho] wa ambaye hakuliinulia hilo kichwa na wala hakuukubali uongofu wa Allaah niliotumwa nao.”[2]
Hapa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kawagawa watu kwa kuzingatia uongofu na elimu katika mafungu matatu.
[1] 13:17
[2] al-Bukhaariy (79) na Muslim (2282).
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 133-135
- Imechapishwa: 26/08/2025

Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 133-135
Imechapishwa: 26/08/2025
https://firqatunnajia.com/74-maji-safi-yanapita-chini-ya-povu/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket