73 – Mu´aadh bin Jabal amesimulia kuwa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Wale wanaopendana kwa ajili ya Allaah atawaweka chini ya kivuli cha ´Arshi Yake Siku ambayo hakuna kivuli kingine isipokuwa kivuli Chake.”[1]
[1] Swahiyh. Ameipokea Ahmad (5/229, 236 na 237), Ibn Hibbaan (2510), al-Haakim (4/169-170) na Ibn-ul-Mubaarak katika “az-Zuhd” (715) kupitia njia mbili zingine Swahiyh. Moja katika njia hizo mbili ameisahihisha al-Haakim kwa mujibu wa sharti za al-Bukhaariy na Muslim na adh-Dhahabiy akaafikiana naye. Hata hivyo usahihishaji huo unatakiwa kuangaliwa vyema, kama nilivyobainisha katika “Swahiyh-ut-Targhiyb wat-Tarhiyb” (4/47).
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Mukhtasar-ul-´Uluww, uk. 112-113
- Imechapishwa: 26/06/2024
- Taaliki: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket