Ama mnafiki moyo wake ni kipofu, haujapita macho yake giza na hajaona isipokuwa umeme unaokaribia kupofua macho, radi kubwa na giza. Kwa hiyo ameingiwa na khofu na akaliogopa hilo. Matokeo yake akajiziba masikio yake kwa vidole vyake ili asisikie sauti ya radi. Akatishwa na umeme huo na nguvu ya mng’ao wake na ukubwa wa nuru yake. Kwa hiyo anaogopa kwamba umeme huo utamchukua macho yake, kwa sababu macho yake ni dhaifu hayawezi kustahimili hiyo nuru. Yupo katika giza akisikia sauti ya radi kali na anaona umeme mkali wa kushitua. Ikiwa umeme huo umeangaza kati ya mbele yake anatembea ndani ya mwangaza huo. Akipoteza nuru hiyo anasimama hali ya kukanganyikiwa na hajui aende wapi. Kwa sababu ya ujinga wake hajui kuwa hilo ni miongoni mwa lazima ya mvua ambayo kwayo hupatikana uhai wa ardhi na mimea na uhai wake yeye mwenyewe. Bali anachoelewa ni radi, umeme na giza tu. Hana hisia na yaliyoko nyuma ya hayo. Basi uoga ni wa lazima kwake. Khofu na woga havitengani naye.
Ama yule aliyezoea mvua mkali na anajua kuwa ni lazima kuwe na radi, umeme na giza kwa sababu ya mawingu, basi huona faraja kwa hilo, haingiwi na khofu wala halimkatazi hilo kuchukua fungu lake katika mvua hiyo.
Huu ni mfano unaolingana kabisa na ile mvua iliyoteremshwa na Jibriyl (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutoka kwa Mola wa walimwengu wote (Tabaarak wa Ta´ala) juu ya moyo wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ili kuhuisha kwao nyoyo na ulimwengu wote. Hekima Yake ilihukumu kwamba uambatane na hilo mvua kutoka mawinguni, ngurumo na radi mfano wa mvua ya maji. Ni hukumu za kina na sababu zilizopangiliwa kwa mpangilio wa yule ambaye ni Mshindi na Mwenye hekima.
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 129-130
- Imechapishwa: 26/08/2025
Ama mnafiki moyo wake ni kipofu, haujapita macho yake giza na hajaona isipokuwa umeme unaokaribia kupofua macho, radi kubwa na giza. Kwa hiyo ameingiwa na khofu na akaliogopa hilo. Matokeo yake akajiziba masikio yake kwa vidole vyake ili asisikie sauti ya radi. Akatishwa na umeme huo na nguvu ya mng’ao wake na ukubwa wa nuru yake. Kwa hiyo anaogopa kwamba umeme huo utamchukua macho yake, kwa sababu macho yake ni dhaifu hayawezi kustahimili hiyo nuru. Yupo katika giza akisikia sauti ya radi kali na anaona umeme mkali wa kushitua. Ikiwa umeme huo umeangaza kati ya mbele yake anatembea ndani ya mwangaza huo. Akipoteza nuru hiyo anasimama hali ya kukanganyikiwa na hajui aende wapi. Kwa sababu ya ujinga wake hajui kuwa hilo ni miongoni mwa lazima ya mvua ambayo kwayo hupatikana uhai wa ardhi na mimea na uhai wake yeye mwenyewe. Bali anachoelewa ni radi, umeme na giza tu. Hana hisia na yaliyoko nyuma ya hayo. Basi uoga ni wa lazima kwake. Khofu na woga havitengani naye.
Ama yule aliyezoea mvua mkali na anajua kuwa ni lazima kuwe na radi, umeme na giza kwa sababu ya mawingu, basi huona faraja kwa hilo, haingiwi na khofu wala halimkatazi hilo kuchukua fungu lake katika mvua hiyo.
Huu ni mfano unaolingana kabisa na ile mvua iliyoteremshwa na Jibriyl (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kutoka kwa Mola wa walimwengu wote (Tabaarak wa Ta´ala) juu ya moyo wa Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ili kuhuisha kwao nyoyo na ulimwengu wote. Hekima Yake ilihukumu kwamba uambatane na hilo mvua kutoka mawinguni, ngurumo na radi mfano wa mvua ya maji. Ni hukumu za kina na sababu zilizopangiliwa kwa mpangilio wa yule ambaye ni Mshindi na Mwenye hekima.
Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 129-130
Imechapishwa: 26/08/2025
https://firqatunnajia.com/72-zowea-mvua-kali-ya-dhoruba/