Ahl-ul-Bid´ah wameijibu Hadiyth kuhusu mjakazi pale ambapo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomuuliza: “Allaah yuko wapi?” Akasema: “Mbinguni.” Akamuuliza: “Mimi ni nani?” Akasema: “Mtume wa Allaah.” Akasema: “Mwache huru! Kwani hakika ni muumini.” Muslim (537), Abu Daawuud (920), (3282), Ahmad (05/447-448), Ibn Abiy ´Aaswim (104), at-Twabaraaniy katika “al-Kabiyr” (19/938), Ibn Hibbaan katika “as-Swahiyh” yake (165).
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamshuhudia ya kwamba ni muumini.
Ahl-ul-Bid´ah wameyajibu haya na kusema kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliulizwa swali bovu. Ameulizwa hivyo kwa sababu ndio [swali] linaloendana na akili na uelewa wa yule mjakazi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anataka kumwambia:
“Allaah ni nani?”
‘Hakuwa anakusudia kusema:
“Allaah yuko wapi?”
Wanasema kuwa hakuulizwi Allaah yuko wapi. Wanasema kuwa “wapi” kunaulizwa kuhusu sehemu. Hivyo wewe ukisema “wapi” basi unataka kumfanya Allaah kuwa sehemu, kuwa na kikomo na mpaka. Kusema hivi kwa madai yao ni kumtukana Allaah na hivyo ni ukafiri. Anayethibitisha kwamba Allaah yuko juu wanasema kuwa ni kafiri. Wanasema ni kwa sababu amemtukana Allaah kwa kumfanya kuwa sehemu. Kwa mujibu wao Allaah yuko katika kila pande na hana kikomo sehemu moja. Wanasema kuwa kilichoko sehemu ni kiwiliwili, kilicho na kikomo, kilicho na mpaka ni kiumbe. Kitu kama hichi ndicho kinachokuwa pahala. Mwenye kusema kuwa Allaah yuko sehemu huyo amemtukana na anayemtukana Allaah amekufuru. Kwa ajili hii ndio maana wamemkufurisha mwenye kuthibitisha Ujuu.
Vilevile wanasema haifai kuashiria kwa kidole kwamba Allaah yuko mbinguni. Hawakubali kuashiria kwa kihisia. Lau utaashiria kwa kidole mbinguni na mtu Jahmiy yuko karibu na wewe basi atakikata kidole chako papo hapo. Tahadhari kuashiria kidole chako kukielekeza mbinguni na wewe uko karibu na mtu Jahmiy. Anaweza kukikata kidole chako papo hapo kwa sababu anaona kuwa wewe ni kafiri na ni Mujassim mwenye kumtukana Allaah.
- Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh al-Qaa´idah al-Marraakushiyyah, uk. 45
- Imechapishwa: 30/04/2020

Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh al-Qaa´idah al-Marraakushiyyah, uk. 45
Imechapishwa: 30/04/2020
https://firqatunnajia.com/71192-2/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)