03 – Kula au kunywa. Nako ni kule kukifikisha chakula au kinywaji tumboni kwa njia ya mdomo au pua. Haijalishi kitu ile aina ya chakula au kinywaji. Amesema (Ta´ala):

وَكُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّىٰ يَتَبَيَّنَ لَكُمُ الْخَيْطُ الْأَبْيَضُ مِنَ الْخَيْطِ الْأَسْوَدِ مِنَ الْفَجْرِۖ ثُمَّ أَتِمُّوا الصِّيَامَ إِلَى اللَّيْلِ

“Kuleni na kunyweni mpaka ubainike kwenu weupe wa alfajiri katika weusi wa usiku. Kisha timizeni swawm mpaka usiku.”[1]

Kuweka ugoro puani ni kama kula na kunywa. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kupitia kwa Laqiytw bin Swabirah:

“Fanya kishindo katika kuyapindisha maji puani isipokuwa ukiwa umefunga.”

Wameipokea watano na ameisahihisha at-Tirmidhiy.

Kuhusu kunusa harufu mbalimbali hakumfunguzi mtu kwa sababu hakuna virutubisho vinavyoingia tumboni.

[1] 02:187

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majaalis Shahr Ramadhwaan, uk. 99-100
  • Imechapishwa: 23/02/2024