Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
122 – Tunaamini zile karama zilizopokelewa kutoka kwao na zikasihi kupitia wapokezi wenye kuaminika.
MAELEZO
Mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) amefanya vizuri kufungamanisha maneno yake ”kwa wapokezi wenye kuaminika”. Kwa sababu watu, khaswa wa zama hizi, wameenda mbali zaidi juu ya masimulizi yanayozungumzia karama mpaka kufikia kiasi cha kwamba wanayasimulia mambo ya batili kabisa ambayo hakuna yeyote mwenye akili kidogo kabisa anayetilia shaka juu ya ubatilifu wake. Bali wakati mwingine yanakuwa na shirki kubwa inayohusiana na uola wa Allaah. Kitabu ”Twaqabaat-ul-Awliyaa” cha ash-Sha´raaniy ni moja katika vitabu vinavyoingia kwa ndani zaidi kutaja mambo hayo ya batili. Humo amesema mmoja katika mawalii:
”Kwa miaka ishirini nimeacha kukiambia kitu ”Kuwa!” – na hivo kwa ajili ya kufanya adabu kwa Allaah.”
Allaah ametakasika kukubwa kutokana na wanayoyasema!
Upande mwingine utapata mapokezi kadhaa sahihi kuhusu karama za baadhi ya Maswahabah katika kitabu “Riyaadh-us-Swaalihiyn”[1] cha Imaam an-Nawawiy.
[1] Tazama ukaguzi wangu wa “Riyaadh-us-Swaalihiyn” (1516-1523).
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah – Sharh wa Ta´liyq, uk. 106-107
- Imechapishwa: 20/10/2024
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket