Amefananisha (Ta´ala) hali ya wanaafiki walipotoka katika nuru baada ya kuangaziwa nayo na hali ya aliyewasha moto kisha nuru yake ikaondolewa baada ya kuangaza yaliyomzunguka, kwa sababu wanaafiki kwa kuchanganyika kwao na waislamu, kuswali pamoja nao, kufunga pamoja nao, kusikia kwao Qur-aan na kushuhudia kwao alama za Uislamu na nguzo zake wameona mwanga na wameuona kwa macho nuru. Kwa ajili hiyo Allaah (Ta´ala) amesema juu yao:
صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لَا يَرْجِعُونَ
”… viziwi, mabubu, vipofu basi hawatorejea.”[1]
Kwa sababu wameuacha Uislamu baada ya kuwa ndani yake na kunufaika nao. Kwa ajili hiyo hawarudi tena. Allaah (Ta´ala) amesema juu ya makafiri:
صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لَا يَعْقِلُونَ
“… viziwi, mabubu, vipofu kwa hiyo hawaelewi!”[2]
Kwa sababu hawakuelewa Uislamu, kuingia ndani yake wala kufaidika nao, bali bado wako katika giza la ukafiri – ni viziwi, mabubu na vipofu.
Ametakasika kutokana na mapungufu Yule ambaye amefanya maneno Yake kuwa tiba kwa magonjwa ya vifua, wito kwa ajili ya imani na hakika zake, mwaliko wa maisha ya milele na neema isiyokatika na uongozi kuelekea njia ya uongofu. Kwa hakika mwita wa imani amewasikilizisha wenye kusikia lau kama wangekuwa na masikio yenye kuelewa na mawaidha ya Qur-aan yangeponya lau yangelikutana na nyoyo tupu, lakini pepo za mashaka na matamanio zimevuma juu ya nyoyo na kuzizima taa zake, mikono ya kughafilika na ujinga imezitawala na kufunga milango ya uongofu wake na kupoteza funguo zake, matendo yake yamefanya kifuniko, basi maneno hayafai kitu juu yake. Zimelewa kwa matamanio ya upotovu na ushuhuda wa batili, basi hazisikii lawama tena. Zimepewa mawaidha ambayo mikuki na mishale ingeathiri zaidi. Hata hivyo zimekufa ndani ya bahari ya ujinga na kughafilika na kifungo cha matamanio na shahawa, lakini jeraha halimuumi mfu!
[1] 02:18
[2] 02:171
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 126-127
- Imechapishwa: 25/08/2025
Amefananisha (Ta´ala) hali ya wanaafiki walipotoka katika nuru baada ya kuangaziwa nayo na hali ya aliyewasha moto kisha nuru yake ikaondolewa baada ya kuangaza yaliyomzunguka, kwa sababu wanaafiki kwa kuchanganyika kwao na waislamu, kuswali pamoja nao, kufunga pamoja nao, kusikia kwao Qur-aan na kushuhudia kwao alama za Uislamu na nguzo zake wameona mwanga na wameuona kwa macho nuru. Kwa ajili hiyo Allaah (Ta´ala) amesema juu yao:
صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لَا يَرْجِعُونَ
”… viziwi, mabubu, vipofu basi hawatorejea.”[1]
Kwa sababu wameuacha Uislamu baada ya kuwa ndani yake na kunufaika nao. Kwa ajili hiyo hawarudi tena. Allaah (Ta´ala) amesema juu ya makafiri:
صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لَا يَعْقِلُونَ
“… viziwi, mabubu, vipofu kwa hiyo hawaelewi!”[2]
Kwa sababu hawakuelewa Uislamu, kuingia ndani yake wala kufaidika nao, bali bado wako katika giza la ukafiri – ni viziwi, mabubu na vipofu.
Ametakasika kutokana na mapungufu Yule ambaye amefanya maneno Yake kuwa tiba kwa magonjwa ya vifua, wito kwa ajili ya imani na hakika zake, mwaliko wa maisha ya milele na neema isiyokatika na uongozi kuelekea njia ya uongofu. Kwa hakika mwita wa imani amewasikilizisha wenye kusikia lau kama wangekuwa na masikio yenye kuelewa na mawaidha ya Qur-aan yangeponya lau yangelikutana na nyoyo tupu, lakini pepo za mashaka na matamanio zimevuma juu ya nyoyo na kuzizima taa zake, mikono ya kughafilika na ujinga imezitawala na kufunga milango ya uongofu wake na kupoteza funguo zake, matendo yake yamefanya kifuniko, basi maneno hayafai kitu juu yake. Zimelewa kwa matamanio ya upotovu na ushuhuda wa batili, basi hazisikii lawama tena. Zimepewa mawaidha ambayo mikuki na mishale ingeathiri zaidi. Hata hivyo zimekufa ndani ya bahari ya ujinga na kughafilika na kifungo cha matamanio na shahawa, lakini jeraha halimuumi mfu!
[1] 02:18
[2] 02:171
Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 126-127
Imechapishwa: 25/08/2025
https://firqatunnajia.com/70-lakini-jeraha-halimuumi-mfu/