Shaykh-ul-Islaam Ahmad bin Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:
Aina hii ya makadirio wanaikadhibisha Qadariyyah wote ambao Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewaita kuwa ni:
“Waabudia moto wa ummah huu.”[1]
Wako wengine pia ambao wameithibitisha kwa kupindukia mipaka mpaka wakamkanushia mja uwezo na utashi wake na isitoshe wakazitoa hekima na manufaa kutoka katika matendo na hukumu za Allaah.
MAELEZO
Hapo zamani Qadariyyah waliopindukia walikuwa wakipinga daraja ya kwanza ambayo ni elimu ya Allaah. Baada ya hapo wakajirejea kwa hilo. Leo wanaopinga hilo ni idadi ya watu wachache, kama ambavyo amesema mtunzi (Rahimahu Allaah). Hili ni kuhusiana na elimu ya Allaah juu ya kuyajua mambo na kuyaandika.
Qadariyyah wengi wanapinga daraja ya pili ambayo inahusiana na Allaah kuyaumba mambo na kwamba matakwa Yake ni yenye kutekelezeka. Miongoni mwao ni Mu´tazilah na wengineo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewaita wao kuwa ni:
“Waabudia moto wa ummah huu.”
Waabudia moto ndio wenye kusema ya kwamba ulimwengu una waungu wawili: nuru, ambayo inaumba mambo mazuri, na giza, ambalo linaumba mambo mabaya. Wanaona kuwa waja ndio wenye kuumba matendo yao wenyewe na kwamba hawakutanguliwa kukadiriwa nayo. Wanasema kuwa wao wenyewe ndio wenye kuyafanya na Allaah hakuyaumba. Haya ni kutokana na ujinga na upotevu wao. Hivo ndivo wanavosema Mu´tazilah na Qadariyyah wakanushaji. Kusema kwao hivi ina maana wamemkadhibisha Allaah na Mtume Wake na kwa ajili hiyo wamekuwa makafiri.
Miongoni mwa Qadariyyah kuna wenye kuitwa Jabriyyah. Humo kunaingia pia Jahmiyyah na wenye kufanana nao wenye kusema kwamba mja ni mwenye kutenzwa nguvu na hana uwezo wala khiyari yoyote ya kutenda. Bali ametenzwa nguvu. Watu hawa wamepotea. Nao ni Jahmiyyah wenye kukanusha sifa za Allaah. Wamekusanya kati ya kukanusha sifa za Allaah na imani ya kutenzwa nguvu ambapo wanaona kuwa mja ametenzwa nguvu na hawezi kutenda kwa khiyari. Mapote yote haya yamepotea kuanzia Jahmiyyah, Mu´tazilah, Qadariyyah wakanushaji na Shiy´ah Imaamiyyah kwa sababu na wao ni Mu´tazilah wenye kukanusha makadirio.
[1] Abu Daawuud (4691), Ibn Maajah (92) na al-Haakim (1/85).
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 103-104
- Imechapishwa: 03/11/2024

Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh al-´Aqiydah al-Waasitwiyyah, uk. 103-104
Imechapishwa: 03/11/2024
https://firqatunnajia.com/70-imani-mbili-mbovu-juu-ya-makadirio/