158 – Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza:

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiwakinga al-Hasan na al-Husayn (Radhiya Allaahu ´anhumaa) kwayo na akisema baba zenu wawili walikuwa wakiwaomba kinga kwayo Ismaa´iyl na Ishaaq:

أُعيـذُكُمـا بِكَلِـماتِ اللهِ التّـامَّة، مِنْ كُلِّ شَيْـطانٍ وَهـامَّة، وَمِنْ كُـلِّ عَـيْنٍ لامَّـة

“Nawalinda kwa maneno ya Allaah yaliyokamilika kutokamana na kila shaytwaan na uvamizi na kutokamana na kila jicho lenye kudhuru.”[1]

Ameipokea al-Bukhaariy.

MAELEZO

Katika Hadiyth hii kuna kusuniwa kuomba kinga na ulinzi kwa maneno ya Allaah.

Vilevile kuna dalili ya kwamba maneno ya Allaah sio kiumbe.

Aidha kuna Radd kwa Mu´tazilah na Ahl-ul-Bid´ah wengine wanaosema kuwa maneno ya Allaah ni kiumbe. Kwa sababu Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hawezi kuomba kinga kwa viumbe. Kwa hivyo haifai kuomba kinga isipokuwa kwa Allaah, kwa sababu kuomba ulinzi ni ´ibaadah. ´Ibaadah hatekelezewi yeyote isipokuwa Allaah (´Azza wa Jall).

Hapa ndipo mwisho na himdi zote njema ni stahiki ya Allaah.

[1] al-Bukhaariy (3371).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 150
  • Imechapishwa: 16/11/2025