Kutokana na hilo Yeye (Subhaanah) amepiga mifano miwli, moja wa maji na mwingine wa moto. Kwa sababu maji yanapeleke katika uhai na moto unapelekea kuangaza na nuru. Mfano huo ameupiga mwanzoni mwa Suurah ”al-Baqarah” pale aliposema:
مَثَلُهُمْ كَمَثَلِ الَّذِي اسْتَوْقَدَ نَارًا فَلَمَّا أَضَاءَتْ مَا حَوْلَهُ ذَهَبَ اللَّـهُ بِنُورِهِمْ وَتَرَكَهُمْ فِي ظُلُمَاتٍ لَّا يُبْصِرُونَ
”Mfano wao ni kama mfano wa aliyekoka moto. Ulipoyaangaza yaliyo pembezoni mwake, AllaahaAkawaondoshea nuru yao na akawaacha katika viza hali ya kuwa hawaoni.”[1]
Amesema kuwa ”ameondoa nuru yao” na hausema moto wao. Kwa sababu moto una uchomaji.
Vivyo hivyo inapokuja kwa wanafiki; nuru ya imani yao imeondoka kwa sababu ya unafiki na kilichosalia katika nyoyo zao ni joto la ukafiri, mashaka na shubuha vikichemka ndani ya nyoyo zao. Nyoyo zao zimechomwa na joto lake, maudhi yake, sumu zake na miale yake ulimwenguni, basi Allaah (Ta´ala) atawaingiza humo siku ya Qiyaamah Moto uliowashwa na wenye kupenya hadi kwenye vifua. Huu ndio mfano wa yule ambaye nuru ya imani haikumsindikiza duniani, bali ilimtoka na kumwacha baada ya kunufaika nayo kwa muda. Hivo ndivyo ilivyo hali ya mnafiki; alitambua kisha akakataa, alikiri kisha akakanusha. Basi yuko katika giza, kiziwi, bubu na kipofu, kama alivyosema (Ta´ala) kuhusu ndugu zao makafiri:
وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا صُمٌّ وَبُكْمٌ فِي الظُّلُمَاتِ ۗ مَن يَشَإِ اللَّـهُ يُضْلِلْـهُ وَمَن يَشَأْ يَجْعَلْهُ عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ
”Wale waliokadhibisha Aayah Zetu ni viziwi na mabubu waliyo ndani ndani ya viza. Allaah humpotoa amtakaye na humuweka amtakaye juu ya njia iliyonyooka.”[2]
وَمَثَلُ الَّذِينَ كَفَرُوا كَمَثَلِ الَّذِي يَنْعِقُ بِمَا لَا يَسْمَعُ إِلَّا دُعَاءً وَنِدَاءً ۚ صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لَا يَعْقِلُونَ
“Na mfano wa wale waliokufuru ni kama mfano wa yule ambaye anapiga kelele kwa asiyesikia ila wito na kelele tu [za wanyama anaowachunga]; viziwi, mabubu, vipofu kwa hiyo hawaelewi!”[3]
[1] 2:17
[2] 6:39
[3] 02:171
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 125-126
- Imechapishwa: 25/08/2025
Kutokana na hilo Yeye (Subhaanah) amepiga mifano miwli, moja wa maji na mwingine wa moto. Kwa sababu maji yanapeleke katika uhai na moto unapelekea kuangaza na nuru. Mfano huo ameupiga mwanzoni mwa Suurah ”al-Baqarah” pale aliposema:
مَثَلُهُمْ كَمَثَلِ الَّذِي اسْتَوْقَدَ نَارًا فَلَمَّا أَضَاءَتْ مَا حَوْلَهُ ذَهَبَ اللَّـهُ بِنُورِهِمْ وَتَرَكَهُمْ فِي ظُلُمَاتٍ لَّا يُبْصِرُونَ
”Mfano wao ni kama mfano wa aliyekoka moto. Ulipoyaangaza yaliyo pembezoni mwake, AllaahaAkawaondoshea nuru yao na akawaacha katika viza hali ya kuwa hawaoni.”[1]
Amesema kuwa ”ameondoa nuru yao” na hausema moto wao. Kwa sababu moto una uchomaji.
Vivyo hivyo inapokuja kwa wanafiki; nuru ya imani yao imeondoka kwa sababu ya unafiki na kilichosalia katika nyoyo zao ni joto la ukafiri, mashaka na shubuha vikichemka ndani ya nyoyo zao. Nyoyo zao zimechomwa na joto lake, maudhi yake, sumu zake na miale yake ulimwenguni, basi Allaah (Ta´ala) atawaingiza humo siku ya Qiyaamah Moto uliowashwa na wenye kupenya hadi kwenye vifua. Huu ndio mfano wa yule ambaye nuru ya imani haikumsindikiza duniani, bali ilimtoka na kumwacha baada ya kunufaika nayo kwa muda. Hivo ndivyo ilivyo hali ya mnafiki; alitambua kisha akakataa, alikiri kisha akakanusha. Basi yuko katika giza, kiziwi, bubu na kipofu, kama alivyosema (Ta´ala) kuhusu ndugu zao makafiri:
وَالَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا صُمٌّ وَبُكْمٌ فِي الظُّلُمَاتِ ۗ مَن يَشَإِ اللَّـهُ يُضْلِلْـهُ وَمَن يَشَأْ يَجْعَلْهُ عَلَىٰ صِرَاطٍ مُّسْتَقِيمٍ
”Wale waliokadhibisha Aayah Zetu ni viziwi na mabubu waliyo ndani ndani ya viza. Allaah humpotoa amtakaye na humuweka amtakaye juu ya njia iliyonyooka.”[2]
وَمَثَلُ الَّذِينَ كَفَرُوا كَمَثَلِ الَّذِي يَنْعِقُ بِمَا لَا يَسْمَعُ إِلَّا دُعَاءً وَنِدَاءً ۚ صُمٌّ بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لَا يَعْقِلُونَ
“Na mfano wa wale waliokufuru ni kama mfano wa yule ambaye anapiga kelele kwa asiyesikia ila wito na kelele tu [za wanyama anaowachunga]; viziwi, mabubu, vipofu kwa hiyo hawaelewi!”[3]
[1] 2:17
[2] 6:39
[3] 02:171
Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 125-126
Imechapishwa: 25/08/2025
https://firqatunnajia.com/69-moto-na-maji/