68. Ni ipi hukumu ya kusoma kwa mwalimu ambaye ana ´Aqiydah tofauti na Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah inapokuja katika majina na sifa za Allaah?

Swali 68: Ni ipi hukumu ya kusoma kwa mwalimu ambaye ana ´Aqiydah tofauti na Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah inapokuja katika majina na sifa za Allaah?

Jibu: Kuchagua mwalimu ambaye amenyooka katika ´Aqiydah na elimu yake ni jambo linalotakikana. Isipowezekana na huyu akawa anafunza kwa mfano Fiqh, sarufi na maudhui mengine yasiyokuwa na uhusiano na ´Aqiydah, basi haina neno kusoma kwake katika zile mada anazoziweza vizuri. Kuhusu ´Aqiydah usiisome isipokuwa tu kwa wale watu walio na ´Aqiydah sahihi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ajwibah al-Mufiydah ´an As-ilat-il-Manaahij al-Jadiydah, uk. 175-176
  • Imechapishwa: 01/07/2024
  • taaliki: Shaykh Jamaal bin Furahyaan al-Haarithiy