Atakapofika Muhassir, ataenda kwa haraka kiasi cha kurusha jiwe, mpaka atakapofika Minaa. Kisha ataanza kwa kupiga vijiwe kiguzo cha ´Aqabah mara saba. Atakipiga kwa vijiwe vidogo saba. Atasema Takbiyr pamoja na kila jiwe na atainua mikono yake wakati wa kurusha. Ataacha Talbiyah mara tu anapoanza kurusha. Ataingia katikati ya bonde na ataelekea Qiblah, wala hatasimama hapo.
Kisha atachinja Hadiy yake, kisha atanyoa kichwa chake au atapunguza nywele zake. Hapo atakuwa ametoka katika Ihraam na kila kitu kitakuwa kimemruhusu isipokuwa wanawake.
- Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 48
- Imechapishwa: 11/11/2026
Atakapofika Muhassir, ataenda kwa haraka kiasi cha kurusha jiwe, mpaka atakapofika Minaa. Kisha ataanza kwa kupiga vijiwe kiguzo cha ´Aqabah mara saba. Atakipiga kwa vijiwe vidogo saba. Atasema Takbiyr pamoja na kila jiwe na atainua mikono yake wakati wa kurusha. Ataacha Talbiyah mara tu anapoanza kurusha. Ataingia katikati ya bonde na ataelekea Qiblah, wala hatasimama hapo.
Kisha atachinja Hadiy yake, kisha atanyoa kichwa chake au atapunguza nywele zake. Hapo atakuwa ametoka katika Ihraam na kila kitu kitakuwa kimemruhusu isipokuwa wanawake.
Muhusika: Imaam Muwaffaq-ud-Diyn bin Qudaamah al-Maqdisiy (afk. 620)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: ´Umdat-ul-Fiqh, uk. 48
Imechapishwa: 11/11/2026
https://firqatunnajia.com/68-kubaki-minaa/