105 – Inajuzu kuketi karibu na kaburi wakati wa mazishi kwa ajili ya kuwakumbusha waliopo juu ya mauti na yaliyo baada yake. Hilo ni kutokana na Hadiyth ya al-Baraa’ bin ‘Aazib (Radhiya Allaahu ´anh) ambaye ameeleza:
“Tulitoka pamoja na Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) katika jeneza la mmoja wa Answaar. Tulipofika kaburini naye bado hajazikwa. Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akaketi [hali ya kuelekea Qiblah] nasi tukaketi karibu naye kana kwamba ndege wametua juu ya vichwa vyetu. Mkono wake ulikuwa na fimbo akichora ardhini. [Akaanza kuinua macho juu na chini mara tatu], kisha akasema: ”Jilindeni kwa Allaah dhidi ya adhabu ya kaburi” akakariri hivo mara mbili au tatu. Kisha akasema:
[”Ee Allaah! Hakika mimi najilinda Kwako kutokana na adhabu ya kaburi.” [mara tatu.”]
Kisha akasema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Hakika mja muumini anapokuwa katika hali ya kuiaga dunia na kuelekea Aakhirah basi humteremkia Malaika kutoka mbinguni ambao nyuso zao ni nyeupe kama jua wakiwa na sanda kutoka Peponi na manukato kutoka Peponi. Huketi mbali naye umbali wa macho. Kisha anajiwa na Malaika wa mauti (´alayhis-Salaam)[1] na kuketi karibu na kichwa chake na kusema: ”Ee nafsi njema!”
Imekuja katika upokezi mwingine:
”Ee nafsi tulivu!] Toka uende kwenye msamaha na radhi kutoka kwa Allaah.” Roho hiyo hutoka kwa urahisi kama vile tone la maji linavyotiririka kutoka kwenye chupa ambapo Malaika wakaipokea haraka.”
[Imekuja katika upokezi mwingine:
”Hata inapotoka roho yake, huombewa du´aa na kila Malaika aliye baina ya mbingu na ardhi, kila Malaika aliye mbinguni na hufunguliwa milango ya mbingu. Hakuna mlinzi wa mlango isipokuwa humuomba Allaah aipandishe roho yake kupitia kwao.] Ikishachukuliwa hawaiwachi katika mkono wake hata jicho kuzinga mpaka waitwae na kuiweka katika ile sanda na yale manukato. [Hayo ndio maneno Yake (Ta´ala):
تَوَفَّتْهُ رُسُلُنَا وَهُمْ لَا يُفَرِّطُونَ
”… basi wajumbe Wetu humfisha, nao hawazembei.”[2]
Hutoka nayo harufu nzuri zaidi iliyowahi kuonekana juu ya uso wa ardhi. Hupandishwa nayo, hawapiti nayo kwa kundi lolote la Malaika isipokuwa husema: ”Ni roho gani hii nzuri?” Husema: ”Ni fulani bin fulani.” Kwa majina yake mazuri aliyokuwa akiitwa duniani mpaka wafike nayo mbingu ya chini. Huomba idhini ya kufunguliwa ambapo wakafunguliwa. Husindikizwa na Malaika waliokaribishwa katika kila mbingu hadi mbingu ya saba. Kisha Allaah (‘Azza wa Jall) aseme: ”Andikeni kitabu cha mja wangu katika ´Illiyyiyn:
وَمَا أَدْرَاكَ مَا عِلِّيُّونَ كِتَابٌ مَّرْقُومٌيَشْهَدُهُ الْمُقَرَّبُونَ
“Na lipi litakalokujulisha nini hiyo ‘Illiyyuun? Ni Kitabu kimeandikwa na kurekodiwa barabara, watakishuhudia wale waliokurubishwa [kwa Allaah].”[3]
Kwa hiyo kitabu chake huandikwa katika ´Illiyyiyn. Kisha huambiwa: ”Mrudisheni duniani, kwani [Mimi nimewaahidi kwamba] Nimewaumba kutoka humo, humo nitawarudisha na humo Nitawatoa mara nyingine. Akasema: [Hurudishwa ardhini na] roho yake hurudishwa katika kiwiliwili chake. [Akasema: ”Hapo husikia miguu ya viatu vya wenzake wanapoondoka kutoka kwake]. Wanajiliwa na Malaika wawili [wakali wa kukemea], [humkemea] na humketisha na humwambia: ”Nani Mola wako?” Humuuliza: ”Mola wangu ni Allaah”. Humuuliza: ”Dini yako ni ipi?” Humuuliza: ”Dini yangu ni Uislamu.” Humuuliza: ”Ni nani huyu mtu aliyetumwa kwenu?” Husema: ”Huyo ni Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).” Humuuliza: ”Ni yepi matendo yako?” Husema: ”Nilisoma Kitabu cha Allaah, nikakiamini na nikakisadikisha.” [Humkemea tena na humwambia: ”Nani Mola wako? Dini yako ni ipi? Nabii wako ni nani?” – Huo ndio mtihani wa mwisho kuoneshwa muumini. Hapo ndipo Allaah anaposema:
يُثَبِّتُ اللَّـهُ الَّذِينَ آمَنُوا بِالْقَوْلِ الثَّابِتِ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَفِي الْآخِرَةِ
“Allaah huwathibitisha wale walioamini kwa kauli thabiti katika maisha ya duniani na Aakhirah.”[4]
ndio dini yangu na Mtume wangu ni Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Basi mtangazaji atatangaza kutoka mbinguni: ”Mja wangu amesema kweli, mtilieni matandiko kutoka Peponi, mvalisheni kutoka Peponi na mfungulieni mlango wa kuelekea Peponi.” Akasema: ”Atajiliwa na harufu yake na uzuri wake na hupanuliwa kaburi lake umbali wa macho kuweza kuona.”
[Imekuja katika upokezi mwingine:
”Huoneshwa kwake] mtu mzuri wa sura, mzuri wa nguo na mzuri wa harufu. Atamwambia: [”Pata bishara njema za radhi kutoka kwa Allaah na mabustani yenye neema za milele.”] Hii ndio siku yako uliyokuwa ukiahidiwa.” Naye amwambie: ”[Nawa pata bishara njema ya kheri, wewe ni nani? Kwani uso wako ni wa kheri!” Atajibu: ”Mimi ni matendo yako mema. [Ninaapa kwa Allaah sikujui isipokuwa ulikuwa mwepesi katika kumtii Allaah na mvivu katika kumuasi Allaah. Basi Allaah akulipe kheri.] Kisha hufunguliwa mlango kutoka Peponi na mlango kutoka Motoni na kuambiwa: ”Haya ndio yalikuwa makazi yako kama ungemuasi Allaah, lakini Allaah amekupa badala yake hii. Atapoyaona yaliyomo ndani ya Pepo atasema: ”Mola wangu, fanya haraka kuleta Qiyaamah ili nirejee kwa jamaa zangu na mali yangu. [Huambiwa: ”Tulizana.”] Akaendelea kusema: ”Hakika mja kafiri.”
[Imekuja katika upokezi mwingine:
”Hakika mja muovu] anapokuwa katika kuiaga dunia na kuelekea Aakhirah, huteremkiwa na Malaika kutoka mbinguni [wakali na wenye nguvu], weusi wa nyuso, wakiwa na magunia [kutoka Motoni]. Huketi mbali naye kiasi cha macho kuweza kuona. Kisha hujiliwa na Malaika wa mauti hadi aketi juu ya kichwa chake ambapo akasema: ”Ee nafsi mbaya! Toka kwenda kwenye ghadhabu na hasira za Allaah.” Hapo hugawanyika katika mwili wake na huvutwa kama pamba inavyovutwa kutoka kwenye sufu iliyolowa [hukata mishipa na neva]. [Hulaaniwa na kila Malaika baina ya mbingu na ardhi, kila Malaika mbinguni na hufungwa milango ya mbingu. Hakuna wakazi wa mlango wowote isipokuwa wanamuomba Allaah roho hiyo isipande kupitia kwao.] Akaichukua na wanapoitwaa hawaiwachi mkononi hata kwa muda mfupi mpaka waiweke kwenye yale magunia. Hutoka nayo harufu mbaya zaidi ya mzoga wowote uliowahi kupatikana juu ya uso wa ardhi. Hupanda nayo. Wanapopanda nayo hawapiti nayo mbele ya kundi lolote la Malaika isipokuwa husema: ”Ni roho gani hii mbaya?” Husema: ”Ni fulani bin fulani.” Kwa majina yake mabaya aliyokuwa akiitwa duniani. Mpaka wafike nayo mbingu ya chini. Wakaombwa kufunguliwa, lakini wasifunguliwe. Kisha Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasoma:
إِنَّ الَّذِينَ كَذَّبُوا بِآيَاتِنَا وَاسْتَكْبَرُوا عَنْهَا لَا تُفَتَّحُ لَهُمْ أَبْوَابُ السَّمَاءِ وَلَا يَدْخُلُونَ الْجَنَّةَ حَتَّىٰ يَلِجَ الْجَمَلُ فِي سَمِّ الْخِيَاطِ
“Hakika wale waliozikadhibisha Aayah Zetu na wakazifanyia kiburi, hawatofunguliwa milango ya mbingu na wala hawatoingia Peponi mpaka ngamia aingie katika tundu ya sindano.”[5]
Allaah (‘Azza wa Jall) husema: ”Andikeni kitabu chake katika Sijjiyn, katika ardhi ya chini kabisa. Kisha husemwa: ”Mrudisheni mja Wangu duniani, kwani Mimi nimewaahidi kwamba nimewaumba kutoka humo, humo nitawarudisha na humo nitawatoa mara nyingine]. Basi roho yake itupwe [kutoka mbinguni] kwa kutupwa [hadi iangukie mwili wake.] Kisha Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akasoma:
وَمَن يُشْرِكْ بِاللَّـهِ فَكَأَنَّمَا خَرَّ مِنَ السَّمَاءِ فَتَخْطَفُهُ الطَّيْرُ أَوْ تَهْوِي بِهِ الرِّيحُ فِي مَكَانٍ سَحِيقٍ
“Yeyote anayemshirikisha Allaah basi ni kana kwamba ameporomoka kutoka mbinguni wakamnyakua ndege au upepo ukamtupa mahali mbali mno.”[6]
Roho yake irudishwe mwilini.
[”Akasema: ”Hakika husikia miguu ya viatu vya wenzake wanapoondoka kwake]. Hujiliwa na Malaika wawili [wakali wa kukemea], humkemea na humketisha ambapo watamuuliza: ”Nani Mola wako?” [Atasema: ”Ahaa…sijui!” Humuuliza: ”Dini yako ni ipi?” Atasema: ”Ahaa…sijui!”] Humuuliza: ”Ni nani huyu mtu aliyetumwa kwenu?”] Hatoweza kutambua jina lake. Ataulizwa: ”Muhammad?” Atasema: ”Ahaa…sijui! [Niliwasikia watu wakisema hivyo!” Husema: ”Hukujua wala hukusoma!” Atatangaza mtangazaji kutoka mbinguni: ”Amesema uwongo. Mtilieni tandiko kutoka Motoni. Mfungulieni mlango wa kuelekea Motoni.” Basi humpata joto na sumu kutoka huko. Kaburi lake humbana mpaka mbavu zake zikutane. Hujiliwa [Imekuja katika upokzi mwingine: ”Huoneshwa] mtu mbaya wa sura, mbaya wa mavazi, mbaya wa harufu. Atamwambia: ”Pata bishara ovu kwa yale yatakayokuumiza. Hii ndio siku yako uliyokuwa ukiahidiwa.” Naye atasema: [“Nawe pata Allaah akupe bishara ya shari], kwani wewe ni nani? Kwa sababu uso wako ni uso wa mtu anayekuja kwa shari.” Atamwambia: “Mimi ni matendo yako maovu.” [Ninaapa kwa Allaah sikukuona isipokuwa ulikuwa mvivu katika kumtii Allaah na mwenye haraka katika kumuasi Allaah.] [Basi Allaah akulipe kwa shari!” Kisha huletwa mtu kipofu, kiziwi, bubu, akiwa na nyundo kubwa ambayo kama ikipigwa nayo mlima basi ungebadilika kuwa mavumbi. Humpiga nayo ambapo akawa mavumbi. Kisha Allaah humrudisha kama alivyokuwa na akapigwa tena kwa pigo jingine, akapiga ukelele sauti yake husikiwa na kila kitu isipokuwa watu na majini. Kisha hufunguliwa mlango wa Motoni na huwekewa mazulia ya moto wa Motoni.] Husema: “Mola wangu! Usilete Qiyaamah.”
Ameipokea Abu Daawuud (2/281), al-Haakim (1/37-40), at-Twayaalisiy (753) na Ahmad (4/287, 288, 295, 296) ambaye tamko ni lake, vilevile al-Aajurriy katika ”ash-Shariy´ah” (367–370).
an-Nasaa’iy (1/282) na Ibn Maajah (1/469–470) wamepokea sehemu ya kwanza hadi maneno:
”Kana kwamba juu ya vichwa vyetu kuna ndege.”
Huu ni upokezi wa Abu Daawuwd (2/70) kwa mukhtaswari zaidi, na pia Ahmad (4/297). al-Haakim amesema:
“Ni Swahiyh kwa masharti ya al-Bukhaariy na Muslim.”
adh-Dhahabiy akaafikiana naye. Ibn-ul-Qayyim pia ameisahihisha katika ”I´laam-ul-Muwaqqi´iyn” (1/214) na ”Tahdhiyb-us-Sunan” (4/337). Kumenakiliwa usahihishaji wake kutoka kwa Abu Nu´aym na wengine.
[1] Hili ndio jina lake kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah. Kuhusu kumwita ”Israaiyl” ni jambo halina msingi, tofauti na ilivyozoeleka kwa watu. Pengine ni katika simulizi za wana wa israaily.
[2] 06:61
[3] 83:19-21
[4] 14:27
[5] 07:40
[6] 22:31
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 198-202
- Imechapishwa: 11/11/2026

Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Ahkaam-ul-Janaa-iz wa Bid´ahaa, uk. 198-202
Imechapishwa: 11/11/2026
https://firqatunnajia.com/103-kuwakumbusha-wahudhuriaji-wakati-wa-mchakazo-wa-mazishi/